Imewekwa na Mhamed khamis
WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI ABDILAHI JIHAD HASSAN AKIWA AMEBEBA KASA AKIELEKEA BAHARINI KUMACHIA HURU.
Waziri wa Mifugo na
Uvuvi Mh. Abdilahi Jihad Hassan amesema uvuvi haramu ni miongoni mwa
vitendo vinavyokwamisha jitihada za serikali katika utunzaji wa
mazingira na viumbe wa asili wa baharini.
Hayo ameyasema wakati akizungumza katika sherehe za kuwaachia huru kasa huko katika hifadhi ndogo ya viumbe hao nungwi.
Amesema ili kudhibiti
hali hiyo lazima wananchi hasa wavuvi waachane na tabia ya kutumia
mbinu duni ya uvuvi haramu inayochangia kuaharibu mazingira na kupoteza
uhai wa viumbe wanaoishi baharini .
Mh.jihad amesema wakati
umefika kwa jamii kuheshimu sheria zilizopo zikiwemo za uvuvi na
uhifadhi wa mazingira ili matumizi ya rasilimali za bahari ziwe endelevu
kwa maslahi ya wananchi na vizazi vijavyo.
Ametoa wito kwa jamii
kuacha kutumia kasa kama kitoweo kwani kufanya hivyo ni kupoteza jamii
ya viumbe hao muhimu katika ukanda wa bahari ya visiwa vya zanzibar.
Katika Risala ya Jumuiya ya Uhifadhi wa Kasa ya Nungwi “Mnarani Natural Aquarium” imesema
inakabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwemo ukosefu wa elimu ya kisasa
juu ya ufugaji wa viumbe hao,bwawa la kufugia kasa kujaa tope mara kwa
mara pamoja na upungufu wa fedha za kuendeshea miradi ya jumuiya hiyo.
No comments:
Post a Comment