Wednesday, February 6, 2013

Kenya kufunga vidhibiti teknolojia kuzuia hotuba za chuki kwenye mtandao kabla ya uchaguzi

Wakati Kenya ilipofanya uchaguzi wake mkuu mwaka 2007, upenyezaji kwenye intaneti katika nchi ulikuwa chini sana. Lakini leo hii, shukrani kwa kebo za 'fibre optic' na kuongezeka kwa upatikanaji wa simu, Wakenya wengi wanaendesha blogi na wanatumia kikamilifu akaunti za habari za kijamii kama vile Twitter na Facebook.
Programu za kuonyesha kwenye mtandao zimewekwa kuwa sehemu katika uchaguzi wa Kenya unaokuja, ukiwapa fursa watazamaji katika nchi wenye simu kutuma uchunguzi kuhusu udanganyifu au vurugu kwenye makao makuu jijini Nairobi. [ Ripoti ya AFPTV] Play Video
  • Wanaume vijana wakitafuta kwenye intaneti katika duka la huduma za komputa mwezi Juni 2012 mtaa wa Kibera jijini Nairobi. Serikali ya Kenya inafuatilia intaneti kwa ajili ya hotuba za chuki kabla ya uchaguzi wa Machi. [Tony Karumba /AFP]
"Ingawaje tunaona hili kama baraka, pia inaweza kutoa laana na inaweza hata kuharibu utulivu wetu kama tutawaacha watu bila kuwaadhibu ambao wanaendelea kutumia vibaya vyombo vya habari vya kijamii kwa kueneza chuki," alisema Mary Ombara, mkurugenzi wa Kamati ya Uendeshaji ya Taifa kwenye Usimamiaji wa Vyombo vya Habari (NSCMM).
Ingawaje hotuba za chuki za kisiasa zimepungua katika vyombo vikuu vya habari, matumizi ya kauli za kuangamiza kisiasa na uchochezi vinatia hofu kwenye kuongezeka kwake katika vyombo vya habari vya kijamii, Ombara aliiambia Sabahi.
Vurugu za baada ya uchaguzi wa 2007-2008, ujumbe wa maandishi kwenye simu za mkononi ulitumwa kukusanya watu na kushawishi umma, alisema. Vurugu hizo zilisababisha kama watu 1,200 kufa na kama 300,000 kupoteza makaazi, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.
Kwa kuwa na maendeleo ya teknolijia ya hivi sasa na kuongezeka kwa vyombo vya habari vya kijamii, ujumbe wa kushawishi utaweza kuwafikia watu maelfu na kufanya maovu makubwa zaidi.
Ombara alisema NSCMM, katika jitihada zake za kuepuka kurudia vurugu, imeajiri wataalamu kufuatilia shughuli za vyombo vya habari vya kijamii kukamata wakosaji ambao wanaeneza hotuba za chuki za kisiasa. Wataalamu hawa kwa sasa wanachunguza wenye blogi watatu na kupanga gharama za majalada dhidi yao kwa ushawishi wa kisiasa.
Sheria ya 2008 ya Tume ya Taifa ya Ushirikiano na Mshikamano inaeleza kwamba watu wanaweza kushtakiwa kwa hotuba za chuki kama watatumia "hotuba ambazo zinahamasisha au kuhimiza vitendo vya vurugu dhidi ya kundi maalumu, na kuleta hali ya chuki au kutunga habari zisizo za kweli ambazo matokeo yake yanaweza kuiweka tume kwenye uhalifu wa chuki".

Udhibiti wa 'kauli za hatari' kwenye mtandao

Mradi wa Umati, uanzishaji unaoendeshwa na kituo cha iHub cha ubunifu wa teknolojia kilichopo Nairobi, unatumia wafuatiliaji wataalamu na teknolojia ya kisasa kutafuta "kauli za hatari" katika vyombo vya habari vya kijamii.
"Mradi wetu wa shirika unajaribu kufuatilia na kuripoti, kwa mara ya kwanza, jukumu linalofanywa na vyombo vipya vya habari kuhusu uchaguzi wa Kenya," iHub ilisema ilipotoa matokeo ya Oktoba 2012. "Mradi wetu utakuwa na raia katika kiini chake na kutumia teknolojia husika kukusanya, kupanga, kuchambua na kusambaza taarifa ambazo tunapokea."
Mradi wa Umati unalenga "kauli za chuki", ambazo ulizielezwa kidogo tu kama kauli za chuki zenye uwezekano wa kusababisha vurugu. Hatimaye mradi unatarajia kuweka ufafanuzi wa kauli za chuki ambazo zinaweza kujumuishwa kwenye katiba.
Meneja utafiti wa iHub Agnes Crandall alisema mradi, ulifanywa kwa ushirikiano na waandaaji wa mifumo ya kompyuta wa Ushahidi, kuajiri watu watano wakiwakilisha makundi ya makabila makubwa matano nchini Kenya ili kufuatilia mitandao, blogu, vyombo vya habari vya kijamii na majukwaa mengine katika mtandao na kuripoti kauli za hatari kwa viongozi husika.
Crandall alisema taarifa zinazotolewa zinaandikwa kwenye ripoti inayoshirikishwa na wakala wa serikali na wabia wa vyama vya kiraia. "Tunatoa ripoti kwa polisi, Wizara ya Habari, Tume ya Taifa ya Mshikamano na Ushirikiano, na Tume Huru ya Mipaka na Uchaguzi," aliiambia Sabahi. "Kazi yetu ni kuonyesha hali ya hatari."
Katika hotuba yake ya awali ya Oktoba 2012, Umati iligundua kwamba kauli za chuki zilizo nyingi zinatokana na watangazaji wa matukio wasiojulikana, ikimaanisha kwamba watumiaji wanatoa majina yao halisi au majina bandia yanayotambulika katika mitandao yao.
"Kutokuwa na hadhari wakati wa kuongea kwenye mtandao kunaonyesha kwamba waongeaji hawazingatii athari mbaya zinazoletwa na kauli zao, wala hawaogopi kuhusu kuhusishwa na kauli za hatari wanazozitoa," ripoti hiyo ilisema.
Wiki iliyopita, serikali iliufunga ukurasa wa mtandao wa Mashada baada ya Umati kugundua ukurasa huo unatumika kusambaza kauli za chuki.
Pamoja na shughuli za ufuatiliaji, wanablogu wa iHub pia wanahusisha umma na ujumbe unaolenga kupunguza makali ya maoni ya kukasirisha yanayotolewa kwenye mtandao, Crandall alisema.

Kuzuia uhuru wa kujieleza

Ingawa ni muhimu kufuatilia na kukomesha wale wenye uwezo wa kuiingiza nchi katika mzunguko mwingine wa vurugu, Ndung'u Wainaina, mkurugenzi mtendaji wa Kituo cha Kimataifa cha Sera na Mgogoro, alisema kupunguza tamko la chuki hakupaswi kuingilia haki za kikatiba.
"Tunapaswa kuwa makini kutopunguza uhuru wa kujieleza," aliiambia Sabahi. "[Ufuatiliaji] haupaswi kutumika kama kusingizio cha kutishia hoja za ukosoaji za serikali au uanzishaji." Alisema utafiti wa mwisho unapaswa kufanyika kabla washukiwa hawajapelekwa mahakamani au kufungwa kwa tovuti kwa tamko la chuki.
Hata hivyo, Ombara, mkurugenzi wa NSCMM, aliondoa woga kwamba kufuatilia shughuli zinazofanyika katika mtandao kutaingilia haki za Wakenya. "Katika kila tunachokifanya, tunafuata sheria," alisema. "Ambacho hatukipendi ni hali ambayo baadhi ya watu wanafurahia uhuru wao kwa kutumia haki za wengine."

Vyombo vya habari vya kijamii ni upanga wenye makali pande mbili

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Bitange Ndemo alisema inawezekana kutumia vyombo vya habari vya kijamii kushinda uchaguzi kwa amani mwaka huu.
"Teknolojia, hususan vyombo vya habari vya kijamii, mara nyingi ni upanga wenye makali pande mbili," Ndemo aliiambia Sabahi. "Vinaweza kutumika kwa kutolea ujumbe ama chanya au hasi. Ni juu yetu kuhakikisha kwamba tunawajibika kutumia teknolojia kuboresha maendeleo yetu."
Ndemo alisema Wakenya wanapaswa kutumia njia ya mtandao kuwasiliana na viongozi wao na kuwabana kuwajibika kwa ahadi zao, na sio kuchochea hisia zao za kikabila na kisiasa ambazo zinaweza kusababisha vurugu.
Ili kuimarisha amani, aliwaagiza watu binafsi na mashirika kutumia vyombo vya habari vya kijamii kuwaripoti wanaochochea chuki ili kuisaidia serikali kuchukua hatua zinazotakiwa.
Alphonce Juma, mwenye umri wa miaka 27 anayeendesha tovuti ya "my Aspirant my Leader", alisema teknolojia inapaswa kutumika kuuwezesha umma.
"Badala ya kutuma au kuanzisha tovuti ambayo inawachimba Wakenya dhidi ya wenzao, niliamua kuanzisha tovuti ambayo inawaeleza Wakenya kwamba wanataka kujua kuhusu watu wanaogombea nafasi za kisiasa, hivyo wanaweza kuwahusisha na hatimaye kufanya uamuzi wanaouelewa katika sanduku la kura," alisema. "Hivi ndivyo teknolojia inapaswa kuwa."
Juma alisema tovuti yake inatoa shauku ya kisiasa na njia ya kujieleza wao wenyewe wanapoufahamisha umma kuhusu historia za wagombea, motisha wa kufanya kazi serikalini na mifumo ya kisiasa.
"Ninafanya hili kwa mapenzi yangu kwa sababu ninaridhika na kujisikia kwamba ninaisaidia nchi yangu kusonga mbele," alisema. "Jitihada hizi, kama zitafanyika kwa kila mmoja wetu katika mtandao, itasaidia kuweka mzunguko wa vurugu za kisiasa kabatini."

No comments:

Post a Comment