Rais J. K. Kikwete,
Raisi wa Tanzania Jakaya Kikwete siku ya Jumamosi (tarehe 9 Februari) alitoa wito wa kuchukuliwa hatua kali wale wanaohusika na kuziuzia maduka binafsi madawa zilizoibwa kutoka kwa serikali, gazeti la The Guardian la Tanzania liliripoti.
"Serikali haiwezi kuendelea na kununua dawa kwa bei ya juu na hatimaye mzigo huo kuishia mikononi mwa wafanyabiashara wasio na maadili, na kuwaacha wengi, hasa watu wa vijijini, kufa," Kikwete alisema katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Hussein Mwinyi.
Kikwete aliwataka polisi na Wizara ya Afya kushirikiana kuyakagua maduka binafsi ya dawa na kuwatia mbaroni wale wanaouza dawa za umma, gazeti la The Standard la Tanzania liliripoti.
"Hatuwezi kuruhusu hili kuendelea kwa sababu watu wetu wanateseka," Kikwete alisema.
Mwinyi alisoma hotuba ya rais katika uzinduzi wa Idara mpya ya Bohari za Dawa mjini Dar es Salaam. Ghala hilo lilijengwa kwa shilingi bilioni 6.4 (dola milioni 4) kwa msaada kutoka serikali ya Marekani na Mfuko wa Dunia wa Kupambana na UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria.
Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Canada, kwa mashirkiano na Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Kuwashughulikia Watoto, zilitoa shilingi bilioni 4.5 (dola milioni 2.8) kwa ujenzi wa vyumba vya baridi vya kutembea ndani na magari mawili ya majokofu.
No comments:
Post a Comment