5 Februari, 2013 - Saa 08:24 GMT

Abdul Kader Mullah amepatikana na hatia ya mauaji wakati wa vita kati ya
Bangladesh na Pakistan
Jopo maalum linaloskiliza
kesi za uhalifu wa kivita, nchini Bangladesh, limempata na hatia ya
mauaji kiogozi wa chama rasmi cha kiisilamu wakati wa vita vya
Bangladeshi kutoaka uhuru kutoka kwa Pakistan mwaka 1971.
Abdul Kader Mullah, kiongozi wa chama cha Jamaat-e-Islami, amepewa hukumu ya kifungo cha maisha jela.Takriban watu milioni tatu raia wa Bangladesh, waliuawa katika vita hivyo.
Watu kumi na wawili wengi wao viongozi wa chama cha Jamaat, wangali wanakabiliwa na kesi kuhusu vita hivyo. Mmoja kati yao tayari amepokea hukumu ya kunyongwa.
Jopo hilo liliundwa kukabiliana na wale wanaokabiliwa na mashtaka ya kushirikiana na majeshi ya Pakistan wakati wa vita vya 1971. Lakini wakereketwa wanaituhumu serikali kwa kulipiza kisasi.
No comments:
Post a Comment