Friday, February 22, 2013

Mabohora waadhimisha siku ya kuzaliwa kiongozi wao kwa kupanda miti Morogoro

 
Jumuiya ya Mabohora mkoa wa Morogoro imeadhimisha miaka 102 ya kuzaliwa Kiongozi wao mkuu wa Jumuiya hiyo Duniani Syedna Mohammed Burhanuddin kwa kupanda miti mia moja ya aina mbalimbali ikiwemo ya matunda  kwa lengo la kuhifadhi mazingira.
Sheikh Mkuu wa Mabohora Mkoa wa Morogoro, Zoeb Bhai,anasema katika kuadhimisha siku ya kuzaliwa ya kiongozi wao mkuu, wameamua kupanda miti katika maeneo ya viwanja vya manispaa, Shule ya Msingi Bungo na nje ya msikiti wao
Sheikh  wa Jumiya ya Mabohora wa Mkoa wa Morogoro, Zoeb Bhai na wanajumuiya hiyo wanaeleza kuwa kutokana na upendo na kumuenzi kiongozi wao huyo wataendelea kupanda miti mingine mia moja ya aina hiyo katika kijiji cha Mkundi kilichopo katika manispaa hiyo ambacho kimeanza kuathirika kimazingira.
Naye mkurugenzi wa manispaaya Morogoro Jervis Simbeye ameipongeza Jumuiya hiyo ya Mabohora kwa kuadhimisha siku ya kuzaliwa ya kiongozi wao mkuu Duniani kwa kupanda miti.
Monica Lyampawe, TBC Morogoro

No comments:

Post a Comment