22 Februari, 2013 - Saa 10:51 GMT

Vijikaratasi vya uchochezi ndivyo vilitumiwa kuchochea watu wakati wa
ghasia za baada ya uchaguzi 2007
Polisi nchini Kenya wanasema
wamepata vijikaratasi vya uchochezi dhidi ya makabila tofauti katika
baadhi ya sehemu nchini humo, siku chache tuu kabla ya uchaguzi mkuu.
Vijikaratasi vya uchochezi vilitumika pakubwa wakati wa ghasia za uchaguzi mkuu uliokumbwa na utata wa mwaka wa 2007.Pia vingine vilipatikana mjini Mombasa ambako kundi linalotaka kujitenga kutoka Kenya, mkoani Pwani, lina makao yake.
Mjini Kisumu, Polisi ilisema vijikaratasi hivyo vilikuwa vikichochea wakaazi dhidi ya watu kutoka jamii tofauti.
Kimaiyo anasema uchunguzi unaendelea lakini hakuna mshukiwa yoyete aliyekamatwa hadi kufikia sasa.
" Kwa wote wanaotaka kuzua vurugu na uchochezi miongoni mwa wakenya wakati huu wa uchaguzi, tunatoa onyo kuwa mkono mrefu wa serikali utawanasa. " alisema Kimaiyo.
" Maafisa wa Polisi wako katika pembe zote za nchi na wanafanya kazi saa ishirini na nne kuhakikisha wanaochapisha na kusambaza vijikaratasi hivyo wanakamatwa na kushtakiwa." aliongeza Kimaiyo.
Wakati huohuo, watu ishirini na watano wamekamatwa kufuatia visa vya ghasia vilivyoripotiwa katika kampeni za Uchaguzi katika mkoa wa kati na Rift Valley
No comments:
Post a Comment