Mahakama ya Somalia siku ya Jumanne (tarehe 5 Februari) iliwahukumu mwanamke aliyesema alibakwa na vikosi vya ulinzi vya Somalia, na mwandishi wa habari ambaye alimfanyia mahojiano kifungo cha mwaka mmoja gerezani, kwa kusema kuwa walikuwa na hatia ya kuharibu heshima ya taifa.
"Tunamfunga kwa kuzikosea asasi za taifa kwa kudai kuwa alibakwa," hakimu Ahmed Aden Farah aliiambia mahakama mjini Mogadishu, kwa mujibu wa AFP. "Atatumikia mwaka mmoja gerezani baada ya kumaliza kumnyonyesha mtoto wake."
Mwandishi wa habari wa Somalia Abdiasis Abdinuur Ibrahim, ambaye tayari yuko kizuizini, ataanza kutumikia kifungo chake mara moja.
"Mahakama inamuona alizikosea asasi za taifa kwa kutengeneza mahojiano ya uongo na kuingia katika nyumba ya mwanamke wakati mume wake hayupo," hakimu alisema.
Vikundi vya haki vimelaani kesi hiyo kama "imehamasishwa kisiasa".
Washitakiwa wengine watatu, ikiwa ni pamoja na mume wa mwathirika, mwanaume na mwanamke aliyesaidia kumjulisha kwa mwandishi wa habari, walionekana hawana hatia na waliachiwa huru.
Katibu Mkuu wa Chama cha Taifa cha Waandishi wa Habari wa Somalia Mohamed Ibrahim alisema kuwa uamuzi wa mahakama unasikitisha na usio wa haki.
"Mwandishi alikuwa ameshitakiwa kwa kashfa dhidi ya taasisi za serikali, bado leo anakutwa na hatia na kuhukumiwa kwa kuingia ndani ya nyumba ya mwanamke na kumhoji bila mume wake," aliiambia Sabahi. "Mwanasheria [wa Ibrahim] atakata rufaa. Tutashinikiza kesi hii na hatutasita mpaka tufanikiwe kupata haki kwa mwenzetu," alisema. "Hii ni jaribio la kuwanyanyasa na kuwanyamazisha waandishi wa habari."
Ibrahim, ambaye anafanyia kazi vituo kadhaa vya redio vya Somalia pamoja na vyombo vya habari vya kimataifa, alikamatwa siku ya tarehe 10 Januari mjini Mogadishu baada ya kufanya uchunguzi wa unyanyasaji wa kijinsia nchini Somalia.
Afisi ya Kisiasa ya Umoja wa Mataifa kwa Somalia alisema siku ya Ijumaa tarehe 1 Februari kuwa "ilielezea wasiwasi wake kwamba uendeshaji wa kesi katika awamu ya kabla ya mashitaka, hasa kurefushwa kwa uwekwaji kizuizini na (sasa imerekebishwa) ukosefu wa ushauri wa kisheria, kungeweza kuleta athiri hasi" kwa mashitaka.
Shirika la Amnesty International, Waangalizi wa Haki za Binadamu na Tume ya Kuwalinda Waandishi zilisema katika taarifa ya pamoja kwamba "kesi imehusishwa na kuongezeka kwa kuvutia hadhira kutokana na viwango vikubwa vya ubakaji...yakiwemo mashambulizi yanayodaiwa kufanywa na vikosi vya usalama".
Waziri mkuu alisema kuwa kikosi kazi cha watu 13 kitakuwa kikichunguza hususan madai yanayoenea ya ubakaji na unyanyasaji wa kijinsia, na iwapo taratibu sahihi zilifuatwa katika kesi ya Ibrahim. Shirdon alirudia kuelezea kupinga kwake kuwekwa ndani kwa mtu yeyote bila ya kushitakiwa.
"Ukweli wa wazi ni kuwa vurugu za kijinsia dhidi ya wanawake hazikubaliki kabisa kabisa na kamwe hazitapita bila ya mtu kuadhibiwa," alisema. "Hatuwezi kuwa na maendeleo mpaka wale waliotenda makosa hayo wapelekwe mbele ya sheria. Lengo la mwisho la serikali yangu ni kumaliza kabisa tabia hizi za kinyama."
Kikosi kazi kimepewa mamlaka ya miezi mitatu, na imepangwa kutoa hadharani ripoti zinazoelezea kwa urefu mambo waliyoyaona na mapendekezo yao.
Wakati huo huo, mbunge wa Somalia Asha Haji Elmi, ambaye pia ni mke wa waziri mkuu, iliitisha mkutano siku ya Jumatatu huko Mogadishu ili kujadili njia za kuzuia ubakaji na vurugu dhidi ya wanawake, mtandao wa Shabelle Media Network wa Somalia uliripoti.
Wawakilishi kutoka mashirika ya asasi za kijamii na viongozi wa dini walihudhuria mkutano huo na kupaza sauti zao kuunga mkono mpango wa Elmi.
Msemaji wa jumuiya ya Wanazuoni wa Somalia Sheikh Nur Barud Gurhan alitoa wito wa kutekelezwa kwa mipango hiyo kufika hadi mikoani, hasa katika maeneo mapya yaliyokombolewa, kutoa mwamko kwamba ubakaji ni kosa linaloadhibiwa kwa kifo.
"Tunamfunga kwa kuzikosea asasi za taifa kwa kudai kuwa alibakwa," hakimu Ahmed Aden Farah aliiambia mahakama mjini Mogadishu, kwa mujibu wa AFP. "Atatumikia mwaka mmoja gerezani baada ya kumaliza kumnyonyesha mtoto wake."
Mwandishi wa habari wa Somalia Abdiasis Abdinuur Ibrahim, ambaye tayari yuko kizuizini, ataanza kutumikia kifungo chake mara moja.
"Mahakama inamuona alizikosea asasi za taifa kwa kutengeneza mahojiano ya uongo na kuingia katika nyumba ya mwanamke wakati mume wake hayupo," hakimu alisema.
Vikundi vya haki vimelaani kesi hiyo kama "imehamasishwa kisiasa".
Washitakiwa wengine watatu, ikiwa ni pamoja na mume wa mwathirika, mwanaume na mwanamke aliyesaidia kumjulisha kwa mwandishi wa habari, walionekana hawana hatia na waliachiwa huru.
Katibu Mkuu wa Chama cha Taifa cha Waandishi wa Habari wa Somalia Mohamed Ibrahim alisema kuwa uamuzi wa mahakama unasikitisha na usio wa haki.
"Mwandishi alikuwa ameshitakiwa kwa kashfa dhidi ya taasisi za serikali, bado leo anakutwa na hatia na kuhukumiwa kwa kuingia ndani ya nyumba ya mwanamke na kumhoji bila mume wake," aliiambia Sabahi. "Mwanasheria [wa Ibrahim] atakata rufaa. Tutashinikiza kesi hii na hatutasita mpaka tufanikiwe kupata haki kwa mwenzetu," alisema. "Hii ni jaribio la kuwanyanyasa na kuwanyamazisha waandishi wa habari."
Ibrahim, ambaye anafanyia kazi vituo kadhaa vya redio vya Somalia pamoja na vyombo vya habari vya kimataifa, alikamatwa siku ya tarehe 10 Januari mjini Mogadishu baada ya kufanya uchunguzi wa unyanyasaji wa kijinsia nchini Somalia.
Afisi ya Kisiasa ya Umoja wa Mataifa kwa Somalia alisema siku ya Ijumaa tarehe 1 Februari kuwa "ilielezea wasiwasi wake kwamba uendeshaji wa kesi katika awamu ya kabla ya mashitaka, hasa kurefushwa kwa uwekwaji kizuizini na (sasa imerekebishwa) ukosefu wa ushauri wa kisheria, kungeweza kuleta athiri hasi" kwa mashitaka.
Shirika la Amnesty International, Waangalizi wa Haki za Binadamu na Tume ya Kuwalinda Waandishi zilisema katika taarifa ya pamoja kwamba "kesi imehusishwa na kuongezeka kwa kuvutia hadhira kutokana na viwango vikubwa vya ubakaji...yakiwemo mashambulizi yanayodaiwa kufanywa na vikosi vya usalama".
Serikali yachukua hatua juu ya haki za binadamu
Pia katika siku hiyo ya Jumanne, Waziri Mkuu Abdi Farah Shirdon pia alizindua kikosi kazi huru cha kushughulikia kile alichokiita "utamaduni wa kutojali" juu ya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Somalia.Waziri mkuu alisema kuwa kikosi kazi cha watu 13 kitakuwa kikichunguza hususan madai yanayoenea ya ubakaji na unyanyasaji wa kijinsia, na iwapo taratibu sahihi zilifuatwa katika kesi ya Ibrahim. Shirdon alirudia kuelezea kupinga kwake kuwekwa ndani kwa mtu yeyote bila ya kushitakiwa.
"Ukweli wa wazi ni kuwa vurugu za kijinsia dhidi ya wanawake hazikubaliki kabisa kabisa na kamwe hazitapita bila ya mtu kuadhibiwa," alisema. "Hatuwezi kuwa na maendeleo mpaka wale waliotenda makosa hayo wapelekwe mbele ya sheria. Lengo la mwisho la serikali yangu ni kumaliza kabisa tabia hizi za kinyama."
Kikosi kazi kimepewa mamlaka ya miezi mitatu, na imepangwa kutoa hadharani ripoti zinazoelezea kwa urefu mambo waliyoyaona na mapendekezo yao.
Wakati huo huo, mbunge wa Somalia Asha Haji Elmi, ambaye pia ni mke wa waziri mkuu, iliitisha mkutano siku ya Jumatatu huko Mogadishu ili kujadili njia za kuzuia ubakaji na vurugu dhidi ya wanawake, mtandao wa Shabelle Media Network wa Somalia uliripoti.
Wawakilishi kutoka mashirika ya asasi za kijamii na viongozi wa dini walihudhuria mkutano huo na kupaza sauti zao kuunga mkono mpango wa Elmi.
Msemaji wa jumuiya ya Wanazuoni wa Somalia Sheikh Nur Barud Gurhan alitoa wito wa kutekelezwa kwa mipango hiyo kufika hadi mikoani, hasa katika maeneo mapya yaliyokombolewa, kutoa mwamko kwamba ubakaji ni kosa linaloadhibiwa kwa kifo.
No comments:
Post a Comment