6 Februari, 2013 - Saa 09:12 GMT

Wanjeshi kutoka Chad walioingia mjini Kidal kusaidiana na jeshi la Ufaransa
Mamia ya wapiganaji wa kiisilamu wameuawa nchini Mali tangu majeshi ya Ufaransa kuanza kupambana nao mwei jana.
Wakati huohuo, waziri wa mambo ya nje Laurent Fabius, amesema kuwa Ufaransa huenda ikaanza kuondoa wanajeshi wake Mali kuanzia mapema mwezi Machi.
Kwenye mahojiano kupitia kwa vyombo vya habari,alisema kuwa ikiwa kila kitu kitakwenda sawa, idadi ya majeshi huenda ikapungua.
Ufaransa ina takriban wanajeshi 4,000 nchini Mali. Hapo jana mkutano wa maafisa kutoka UN, EU na Afrika ulianza mjini Brussels kujadili hatua zitakazochukuliwa baada ya wanjeshi wa Ufaransa kumaliza kazi yao.
Aidha waziri wa ulinzi alisema kuwa mji uliokuwa umesalia kuwa chini ya waasi ,Kidal, tayari umedhibitiwa na majeshi ya Ufaransa.

Maeneo ya milimani ambako wapiganaji wanajificha
Bwana Le Drien alisema kuwa wapiganaji hao walifariki katika mashambulizi ya angani, wengine waliuawa wakiwa kwenye magari yao, na wengine katika mashambulizi ya ardhini mjini Konna mwanzoni mwa kampeini ya kupambana na nao.
No comments:
Post a Comment