Sunday, February 10, 2013

Misri yapiga marufuku Youtube

Mahakama moja ya Misri yamepiga marufuku kwa mwezi mmoja tovuti ya kusambaza video ya Youtube kwa kuonesha filamu iliyotusi Uislamu na kuzusha maandamano ya ghasia katika sehemu kadha za nchi za Kiislamu.
Maandamano ya Karachi kupinga filamu iliyotusi Uislamu mwezi Septemba

Mahakama ya utawala ya Cairo yaliamua kuwa wakuu lazima wachukue hatua kupiga marufuku Youtube nchini na tovuti nyengine yoyote iliyoruhusu filamu hiyo kuoneshwa.
Kesi hiyo ilipelekwa mahakamani na wakili mmoja wa Misri, Hamed Salem, ambaye amewahi kushtaki mashirika mengine ya habari na watu wanaoonekana kuwa wanatusi Uislamu.
Mwezi uliopita mahakama moja ya Misri ilithibitisha hukumu ya kifo kwa Wamisri wasiokuwako mahakamani, kwa kuhusika na filamu hiyo.

No comments:

Post a Comment