Sunday, February 10, 2013

Msichana aliyebakwa azikwa Afrika Kusini


Mamia ya waombolezaji katika mji wa Bredasdorp, jimbo la Western Cape, Afrika Kusini, wamehudhuria mazishi ya msichana aliyebakwa na gengi.
Wanawake vijana wa Afrika Kusini wanakabili tishio la ubakaji
Msichana huyo wa miaka 17 alikutikana ametolewa matumbo kwenye eneo la ujenzi mwisho wa juma lilopita na baadae alifariki hospitalini.
Wanaume watatu wamekamatwa kwa kuhusika na ubakaji na mauaji ya msichana huyo na wanatarajiwa kufikishwa mahakamani juma lijalo.
Shambulio hilo la kikatili limezusha hasira na maandamano kumtaka Rais Jacob Zuma achukue hatua kupambana na visa vingi vya ubakaji nchini Afrika Kusini.

No comments:

Post a Comment