Monday, February 4, 2013

MKURUGENZ MKUU UNESCO AWASILI Z,BAR

 
 
 
 
 
 
Rate This

 Na Hamed Marouy

Mkurugenzi Mkuu wa Unesco Irina Bokova (kulia)akipata maelezo ya Vifaa alivyokuwa akitumia Mfalme Said Bin Sultan kwa Mkurugenzi Idara ya Makumbusho Dk Amina Amei Issa  baada ya kutembelea jumba Wananchi Forodhani ikiwa ni miangoni mwa Ziara yake ya Siku mbili Zanzibar.
 Mkurugenzi Mkuu wa Unesco Irina Bokova (kulia)akipata maelezo ya 
Vifaa alivyokuwa akitumia

 Mfalme Said Bin Sultan kwa Mkurugenzi Idara ya Makumbusho Dk Amina Amei Issa baada ya kutembelea jumba Wananchi Forodhani ikiwa ni miangoni mwa Ziara yake ya Siku mbili Zanzibar.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la elimu, sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO Bi. Irina Bokova amewasili leo Zanzíbar kwa ziara rasmi ya siku mbili.
Mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Amani Karume Bi.Bokova amepokelewa na Mwenyeji wake Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzíbar Ali Juma Shamuhuna.
Kwa mujibu wa Ratiba ya ziara yake Bi.Bokova atafanya atatembelea maeneo mbali mbali ya Mji Mkongwe ikiwa ni pamoja na kukagua Jengo la Makumbusho kuu ya Taifa ambalo lilianguka katika siku za karibuni.
Kesho Bi.Bokova atakuwa na Mazungumzo na Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzíbar wanaohusiana na Ofisi yake ikiwemo Waziri wa Wazira ya Elimu, Waziri wa habari Utamaduni Utalii na Michezo, Waziri wa Ustawi wa Jamii maendeleo ya Wanawake na Watoto na Waziri wa Ardhi Makaazi Maji na Nishati katika Hoteli ya Serena mjini Zanzibar.
Mkurugenzi Mkuu wa Unesco Irina Bokova (kushoto)akiangalia Utamaduni wa Ususi wa Kindu ambazo hutengezewa vitu mbalimbali,makawa, Mikeka hata Mikoba katika moja ya maduka alioingia katika Sehemu za Mji Mkongwe ikiwa ni miangoni mwa Ziara yake ya Siku mbili Zanzibar.
Mkurugenzi Mkuu wa Unesco Irina Bokova (kushoto)akiangalia Utamaduni wa Ususi wa Kindu ambazo hutengezewa vitu mbalimbali,makawa, Mikeka hata Mikoba katika moja ya maduka alioingia katika Sehemu za Mji Mkongwe ikiwa ni miangoni mwa Ziara yake ya Siku mbili Zanzibar.

Aidha Bi. Bokova baada ya Mazungumzo hayo anatarajiwa kufanya Mkutano na Waandishi wa habarí kuhusiana na ziara yake.
Mkurugenzi huyo wa UNESCO atahitimisha ziara yake kwa kumtembelea Rais wa Zanzíbar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein Ofisini kwake.

IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR

No comments:

Post a Comment