5 Februari, 2013 - Saa 07:43 GMT

Rais wa Ufaransa Francois Hollande na makamu wa rais wa Marekani Joe Biden
Maafisa wa Umoja
wa Mataifa, Muungano wa Ulaya na Afrika wanatarajiwa kukutana mjini
Brussels kujadili mkakati wa kuandaa uchaguzi huru na wa kidemokrasia
nchini Mali msimu wa jua.
Pia watajadili hali ya usalama na kibinadamu,
hasa baada ya mapinduzi ya kiraia kufanyika mwaka jana na kufuatiwa na
operesheni ya kijeshi inayoendelea dhidi ya wapiganaji wa kiisilamu.Marekani na Ufaransa, zinataka majeshi ya Afrika kutwaa udhibiti wa eneo hilo kutoka kwa wanajeshi wa Ufaransa.

Kikosi cha wanajeshi wa Mali
Duru zinasema kuwa hatua zinazopigwa na majeshi ya ufaransa zimeweza kusababisha juhudi za kidiplomasia kuhakikisha kuwa usalama wa kudumu unapatikana Mali.
''Wakati nchi inapoporomoka, inachukua muda kuweza kuirejesha katika hali ya kawaida,'' alisema afisaa mmoja mkuu wa Muungano wa Ulaya

Kikundi cha nchi za kigeni ambazo zinaunga mkono Mali, leo kitajadili namna ya kuimarisha mfumo wa kisiasa kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu ambao kaimu rais Dioncounda Traore anatumai utafanyika tarehe 31 mwezi Julai.
Pia itatizama namna ya kufadhili na kutoa mafunzo kwa kikosi cha wanajeshi 8,000 wanaotarajiwa kuchukua nafasi ya wanajeshi wa Ufaransa watakapoondoka.
No comments:
Post a Comment