Wednesday, February 6, 2013

Mwanasiasa wa upinzani auawa Tunisia

 6 Februari, 2013 - Saa 09:43 GMT


Habari za sasa hivi zinasema kuwa kiongozi mkuu wa uopinzani ameuawa kwa kupigwa risasi akiwa anaelekea kazini.
Shrokri Belaeed wa chama cha (Unified Democratic Patriot Party) alipigwa risasi shingoni na kichwani.
Nduguye alithibitisha kuwa bwana Belaid aliyekuwa mratibu wa chama cha Democratic Patriots alifariki baadaye.
Tunisia inakumbwa na mzozo wa kisiasa huku mazungumzo kuhusu mabadiliko katika baraza la mawaziri yakisubiriwa.
Inaarifiwa vyama vingi huenda vikajumuishwa katika muundo wa baraza la mawaziri kwenye serikali ya Muungano inayoongozwa na chama , ingawa mazungumzo kuhusu hili yamekumbwa na hali ya ati ati.

'uhalifu mkubwa'

"Ndugu yangu aliuawa . Nina huzuni mkubwa,'' nduguye marehemu, Abdelmajid Belaid aliambia shirika la habari la AFP .
Haijulikani nani aliyehusika na mauaji hayo.
Duru zinasema kuwa bwana Belaid alikuwa mpinzani mkuu wa serikali iliyoingia mamlakani baada ya mapinduzi ya kiraia mwezi Oktoba mwaka 2011.
Siku ya Jumamosi, aliwatuhumu mamluki waliokodiwa na chama cha Ennahda kwa kuvamia mkutano wa chama chake.
Msemaji wa serikali, Samir Dilou alitaja mauaji hayo kama uhalifu mkubwa .
Nao wanasiasa wa upinzani waliitaja siku ya mauaji kama siku ya huzuni mkubwa Tunisia.

No comments:

Post a Comment