6 Februari, 2013 - Saa 12:24 GMT

Wapiga kura wakijisaji
Wakenya
watakaopokea rushwa kutoka kwa wanasiasa ili kuwapigia kura wakati wa
uchaguzi mkuu mwezi Machi huenda wakajipata matatani.
Kulingana na nakala ya sheria zilizotolewa na
tume huru ya uchaguzi na mipaka , mtu yeyote atakayepokea pesa au
chakula ili kumuunga mkono mgombea fulani, atakuwa anakiuka sheria za
tume hiyo.Kulingana na nakala ya sheria za tume hiyo kuhusu uchaguz, maafisa maalum wa polisi watatateuliwa kutoa usalama wakati wa uchaguzi mkuu mwezi Machi.
Pia nakala hiyo inaelezea kuwa mgombea yopyte atakayetumia rasilimali za serikali kuwalazimisha wapiga kura kuwaunga wagombea fulani au chama fulani cha kisiasa.
Washukiwa wa vitendo hivyo watafikishwa mahakamani huku mkuu wa polisi akisema kesi kama hizo zitachukua miaka mitatu kabla ya hukumu kutolewa.
Yeyote atakayepatikana na hatia huenda akafungwa jela miaka sita au kutozwa faini ya shilingi milioni moja pesa za Kenya. Nchini Kenya ni jambo la kawaida kwa wanasiasa kuwashawishi wapiga kura kwa pesa au chakula ili waweze kuwapigia kura.
No comments:
Post a Comment