Thursday, February 28, 2013

Nec,Zec zatakiwa kujiandaa kusimamia kura ya maoni

 
 
 
 
 
 
Rate This

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na ya Zanzibar (ZEC) zimetakiwa kujipanga na kujiandaa kikamilifu kusimamia zoezi la kupiga kura za maoni katika mchakato wa kupitisha katiba mpya na kupokea mabadiliko kwa mtazamo chanya.
Hayo yalisemwa jijini Dar es Salaam jana na Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe, alipokuwa akifungua mkutano wa Kamati Tendaji za Tume za uchaguzi za nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wenye lengo la kubadilishana mawazo na kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu mifumo ya uchaguzi.
“NEC na ZEC mnatakiwa kujipanga kikamilifu kusimamia zoezi hilo na kupokea mabadiliko kwa mtazamo chanya,” alisema Chikawe.
Katika mchakato wa katiba mpya Tume ya Mabadiliko ya Katiba baada ya kukusanya maoni yaliyotolewa na wananchi kwa sasa inayachambua ili  kuandaa rasimu ya Katiba ifikapo Juni mwaka huu.
Baada ya rasimu hiyo kuandaliwa itapelekwa katika Bunge Maalum la Katiba na Watanzania wote  watapiga kura ya maoni kupitisha katiba hiyo ama kuikataa.
Alisema ingawa ni muhimu kujenga demokrasia, lakini chaguzi za Afrika zimekuwa zikifanyika na wakati mwingine kutokea ugomvi, migogoro na vita inayosababishwa na uwezo mdogo wa kusimamia michakato ya chaguzi.
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment