Thursday, February 28, 2013

TCRL yaifungia Radio Iman kwa madai ya uchochezi

 
 
 
 
 
 
Rate This

tcrl


Mamlaka ya Mawasiliano na Habari nchini Tanzania, TCRA, imetoa adhabu ya kifungo na kulipa faini dhidi ya redio tatu binafsi za nchi hiyo yaani Clouds FM Radio ya jijini Dar es Salaam, Kwa Neema FM Radio ya mjini Mwanza na Radio Imani ya mjini Morogoro kutokana na kurusha matangazo yanayokwenda kinyume na sheria za mamlaka hayo.
Katika adhabu hiyo, Clouds FM imepewa onyo kali la kutokurudia kosa linaloenda kinyume cha sheria za TCRA, pia imeamriwa kulipa faini ya Shilingi milioni 5 kutokana na kutumia kipindi chake cha Power Breakfast kufanya uchochezi na kufuta kipindi chake cha Jicho la Ng’ombe kutokana na sababu za kimaadili.
Faini hiyo inabidi ilipwe mamlaka ya TCRA ndani ya kipindi cha mwezi mmoja kuanzia leo, siku ya kutolewa agizo hilo. Aidha, Kwa Neema FM Radio na Radio Imani zimefungiwa kwa muda wa miezi sita.
Kwa Neema FM imefungiwa kutokana na kuhamasisha na kukuza mgogoro uliozuka hivi karibuni mkoani Geita kuhusu nani mwenye haki ya kuchinja kati ya Waislamu na Wakristo wakati Radio Imani imefungiwa kwa kosa la kuhamasisha watu kususia na kutoshiriki kwenye agizo la Serikali la hesabu ya watu na makazi, Sensa, mwaka 2012

No comments:

Post a Comment