Waziri wa mambo ya Ndani Tanzania Dkt. Emmanuel Nchimbi akifafanua jambo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari
Kwa mujibu wa habari za kuaminika zilizopatikana jana maofisa hao
wako nchini na tayari wamekutana na baadhi ya viongozi wa Serikali kwa
ajili ya kuanza kazi hiyo.
Chanzo chetu cha habari kimeeleza kuwa maofisa hao walikutana na
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi kwa ajili ya
kuangalia ni namna gani watafanya shughuli zao katika upelelezi huo.
Kutua kwa maofisa hao kumekuja baada ya kauli iliyotolewa na Rais
Jakaya Kikwete katika salamu zake za rambirambi baada ya mauaji ya Padri
Mushi kuwa ameliagiza Jeshi la Polisi kutumia nguvu zake zote pamoja na
kushirikiana na vyombo vingine vya usalama vya hapa nchini na mashirika
ya upelelezi ya nchi rafiki katika kufanya uchunguzi wa mauaji hayo.Pamoja na ushiriki wa FBI, pia Serikali inazungumza na nchi nyingine rafiki ili kushirikiana nao katika upelelezi ya matukio mengine ya mauaji ya hivi karibuni.
Taarifa zinaeleza kuwa maofisa wa Serikali wamezungumza na taasisi za
upelelezi za nchi tano ili kuongeza nguvu katika kazi hiyo. Taasisi
nyingine inayotajwa kwamba huenda ikashiriki katika uchunguzi huo ni
Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai ya Uingereza ya Scotland Yard.
Hatua hizi zinakuja baada ya Dk Nchimbi kutoa tamko la Serikali,
Jumapili iliyopita, akidai kuwa mauaji ya Padri Mushi yalikuwa ya
kigaidi hivyo Serikali itachukua hatua kali kuhakikisha waliohusika
wanakamatwa.Haitakuwa mara ya kwanza kwa Serikali ya Tanzania kushirikiana na asasi za kimataifa katika ku chunguza matukio ya uhalifu na yale ya kigaidi. Hii itakuwa mara ya pili kwa FBI kuja nchini kufanya operesheni kubwa ya upelelezi. Mwaka 1998, walifika kuchunguza kulipuliwa kwa Ubalozi wa Marekani na kugundua ilikuwa kazi ya Kundi la Al-Qaeda.
Pia mwaka 1984 walikuja wapelelezi kutoka Scotland Yard kuchunguza kuungua kwa Benki Kuu ya Tanzania (BOT).
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima
alithibitisha Serikali kuanza mazungumzo na mashirika mbalimbali ya
upelelezi duniani kwa ajili ya kushirikiana nayo kuchunguza mauaji ya
Padri Mushi. Alisema tayari wameanza kufanya mazungumzo na mashirika
hayo kutoka nchi mbalimbali, lakini alisema ni mapema mno kuyataja… “Ila
tukikamilisha kila kitu tutawaiteni na kuwaeleza hatua tuliyofikia,
ila tumeanza kufanya mazungumzo nayo. Kama unavyojua Rais Kikwete alitoa
agizo hilo, sisi tumeanza kulitekeleza.” Waziri Silima alisema kwanza
wataanza kuchunguza mauaji ya Padri Mushi… “Tutaanza kuchunguza kwanza
chanzo cha mauaji haya ili tujue kila kitu.”watuhumiwa kukamatwa.Polisi Zanzibar inawashikilia watu kadhaa wakihusishwa na mauaji ya Padri Mushi.
“Tumekamata watu kadhaa kuhusiana na kifo cha Padri na tunaendelea kuwahoji na wengine tutawaachia,” alisema Kamishna wa Polisi wa Zanzibar, Mussa Ali Mussa jana.
No comments:
Post a Comment