Thursday, February 21, 2013

UAMSHO IFUTWE:TAASISI YA UTAWALA BORA TANZANIA (CEGODETA)

 
 
 
 
 
 
Rate This

Baadhi ya Viongozi wa Jumuia ya Uamsho
Baadhi ya Viongozi wa Jumuia ya Uamsho
TAASISI ya Utawala Bora Tanzania (CEGODETA), imeiomba serikali kukipiga marufuku kikundi cha Uamsho na jumuia ya kimataifa itangaze kuwa ni kikundi hatari.

Kauli hiyo ilitolewa na mkurugenzi mtendaji wa taasisi hiyo, Thomas Ngawaiya, kufuatia kuzuka kwa matukio ya mauaji na uharibifu wa mali kwa mgongo wa dini huko visiwani Zanzibar, huku kikundi hicho kikihusishwa kwa ukaribu.

“Kwa kuzingatia hilo CEGODETA, tunaunga mkono tamko lililotolewa na Rais Jakaya Kikwete kwamba uchunguzi wa kina ufanyike ambao utashirikisha mashirika ya nje na wote wanaohusika na mauajji hayo pamoja na wanaofadhili watu wao wachukuliwe hatua za kisheria ili kukata mzizi wa fitina,” alisema.

Ngawaiya aliwatahadharisha Watanzania kutokubali kugawanywa kwa misingi ya dini, ambazo zimeangamiza maisha ya watu wengi katika nchi za Kiislamu duniani.

“Mabomu yamewahi kuua mamia ya watu huko Kenya, Uganda na Sudan kwa sababu ya udini, hadi leo vurugu hizo za mauaji zinaendelea huko kwa kasi.

“Kama Watanzania tusipokuwa makini mambo yaliyotokea kwenye nchi hizo yaweza kutokea hapa kwetu, kwa asiyejua kufa mwambie akatazame kaburi,” alisema.

Aidha aliitaka serikali itoe ulinzi wa kutosha kwa makanisa na viongozi wote wa Kikristo huko Zanzibar, sambamba na bara, pia kwa misikiti na viongozi wa misikiti wanaotishiwa maisha

No comments:

Post a Comment