5 Februari, 2013 - Saa 09:31 GMT

Wanaharakati wakiteta kuhusu dhulma dhidi ya wanawake
Shahidi wa kwanza
katika kesi kuhusu wanaume watano waliombaka na kumuua msichana mmoja
nchini India ameanza kutoa ushahidi wake
Marehemu aliyekuwa na umri wa miaka 23 na
mwanafunzi wa chuo kikuu, alishambuliwa vibaya akiwa ndani ya basi katia
mji mkuu wa India lakini alifariki baadaye kutokana na majeraha
aliyoyapa.Mmoja wa mashahidi wa kwanza kuwasili katika mahakama maalum inayosikiliza kesi hii ya ubakaji mjini Delhi, alikuwa rafiki ya marehemu aliyekuwa naye usiku wa shambulizi hilo.
Aliletwa mahakamani akiwa kwenye kiti cha magurudumu , kwani naye pia alichapwa vibaya sana washukiwa watano waliokamatwa wote walikataa kosa la mauaji , ubakaji na kuharibu ushahidi katika eneo la shambulizi.
Upande wa mashtaka unatarajiwa kuwasilisha mashahidi takriban themanini kuweza wakiwemo madaktari walimtibu marehemu nchini India na India na Singapore, ambako alipelekwa kwa matibabu kujaribu kukoa maisha yake.
Kesi hii inafuatiliwa kwa karibu nchini India ambako ilisababisha maandamano makubwa kuhusu dhulma wanazotendewa wanawake na namna ambavyo polisi na taasisi za kisheria hudhughulikia uhalifu wa
No comments:
Post a Comment