Imeweka na Mhammed khamis
Mkurugenzi
Mkuu wa Unesco Irina Bokova akizungumza na Mawaziri wa Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar huko katika Hoteli ya Serena ikiwa ni muendelezo
wa Ziara yake ya Siku mbili Zanzibar.
Shirika
la Umoja wa Matifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limeahidi
kuendelea kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika
juhudi zake za kuimarisha ustawi wa wananchi kupitia sekta mbali mbali
za maendeleo ikiwemo sekta ya Elimu.
Akizungumza na baadhi ya Mawaziri wa Serikali ambao Wizara zao zinapata misaada kupitia UNESCO, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Bi. Erina Bokova amesema juhudi zinazochukuliwa na Serikali zimepelekea mabadiloko makubwa ya maendeleo visiwani humo.
Amesema UNESCO itaendelea kusaidia sekta ya Elimu kwani inafahamu kwamba kuimarika kwa sekta hiyo ni muelekeo mzuri wa kuimarika kwa sekta nyengine za maendeleo ikiwemo kilimo, utalii na masuala ya Utamaduni nchini.
Ameipongeza Wizara ya Elimu kwa hatua kubwa iliyofikia ya kuwasomesha watoto wote waliofikia umri wa kusoma na ameeleza matumaini yake kwamba sera mpya ya Elimu ya Zanzibar itazidi kuimarika kwa sekta hiyo.
Waziri
wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk kushoto
akipokeya Zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Unesco Irina Bokova
walipomaliza Mazungumzo hapo katika Hoteli ya Serena ikiwa ni muendelezo
wa Ziara yake ya Siku mbili Zanzibar.
Bi.
Erina amesema suala la kuijengea uwezo Wizara ya Elimu na kuwaongezea
ujuzi watendaji wake ni miongoni mwa masuala yatakayoendelea kupewa
kipaumbele na UNESCO.
Akizungumzia
kuimarishwa Mji Mkongwe wa Zanzibar, ambao ni moja kati ya miji
iliyopata heshma ya kuwa ya Urithi wa Kimataifa, Mkurugenzi Mkuu wa
UNESCO amesema hatua ya Serikali kuendelea kuuhifadhi mji huo ni hatua
ya kupigiwa mfano.
Amesema
mabadiliko madogo madogo aliyoyaona katika baadhi ya majengo ya Mji
Mkongwe hayaonyeshi kuondosha mandhari ya asili ya mji huo bali
yanalenga zaidi kubuni vianzio vya ajira kwa wananchi wanaoishi ndani ya
mji huo.
Amesisitiza
kwa Taasisi zinazosimamia Mji huo kuhakikisha kwamba malengo ya
kuufanya mji huo kuwa mji wa urithi wa Kimataifa linaendelezwa na
linasimamiwa vizuri zaidi.
Mkurugenzi
Mkuu wa UNESCO amefurahishwa na uamuzi wa Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar kukubali kuanzishwa kwa vituo vya Redio Jamii Micheweni na
Mtegani Makunduchi na amesema hiyo ni moja ya hatua ya kuwapelekea
maendeleo wananchi wa vijiji hivyo.
Amesema
UNESCO itaendelea kusaidia utaalamu na vifaa mbali mbali kwa vituo
hivyo na vituo vyengine vya aina hiyo ambavyo jamii za vijijini zitaamua
kuvianzisha.
Akizungumza
katika mkutano huo ulioshirikisha wajumbe wa UNESCO na viongozi wa
ngazi za juu wa Serikali katika Hoteli ya Serena Shangani, Waziri wa
Habari, Utamduni, Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk alisema vituo vya
Redio Jamii vimekuwa na mchango mkubwa katika kusukuma mbele maendeleo
ya wanajamii wenyewe.
.Mkurugenzi
Mkuu wa Unesco Irina Bokova katikati akiwa katika Picha ya pamoja na
Mawaziri wa Serikali ya Zanzibar na Viongozi mbalimbali baada ya
kumaliza kwa Mazungumzo yao katika Hoteli ya Serena ikiwa ni muendelezo
wa Ziara yake ya Siku mbili Zanzibar


