Imewekwa na Mhammed Khamis
Jaji mkuu wa Zanzibar Mh, Omar Othman Makungu akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mahakama ya watoto hapa Zanzibar uzinduzi huo.
JAJI
MKUU WA ZANZIBAR MH OMAR OTHMAN MAKUNGU AMESEMA KUANZISHWA KWA MAHAKAMA
YA WATOTO NCHINI KUTASAIDIA KUPUNGUZA MRUNDIKANO WA KESI KATIKA
MAHAKAMA YA MKOA.
AMESEMA
MAHAKAMA HIYO ITAKUWA NA JUKUMU LA KUSHUGHULIKIA KESI ZA JINAI ZINAZO
HUSU WATOTO WALIOCHINI YA UMRI WA MIAKA 18 IKIWA NI UTEKELEZAJI WA
SHERIA NAMBA SITA YA MWAKA 2011 YA SHERIA YA MTOTO ZANZIBAR .
MH MAKUNGU AMEYASEMA HAYO KATIKA UZINDUZI WA MAHAKAMA HIYO ULIYOFANYIKA MAHAKAMA KUU ZANZIBAR VUGA.
AMESEMA LENGO LA KUANZISHWA KWA MAHAKAMA HIYO NI KUTOA HAKI
ZINAZOSTAHILI KWA WATOTO KUTOKANA NA KUONGEZEKA KWA VITENDO VYA
UDHALILISHAJI WANAVYOFANYIWA.
AIDHA
MH MAKUNGU AMESEMA MAHAKAMA HIYO IMEANDAA MAZINGIRA RAFIKI YATAKAYO
MUWEZESHA MTOTO KUJIELEZA KWA UFASAHA WAKATI WA UENDESHWAJI WA KESI HIZO
MAHAKAMANI.
NAE KATIBU MKUU WIZARA YA USTAWI WA JAMII MAENDELEO YA WANAWAKE NA
WATOTO BI FATMA GHARIB BILAL AMEWATAKA WANANCHI KUZITUMIA MAHAKAMA HIZO
KWA KUPELEKA KESI ZINAZO WAHUSU WATOTO ILI KUONDOKANA NA MATATIZO
YANAYOWAKABILI.
MAPEMA
MKURUGENZI WA KITUO CHA HUDUMA ZA SHERIA ZANZIBAR BI, MWANAHARUSI
MIRAJI AMEAHIDI KUWA KITUO HICHO KITAENDELEA KUSHIRIKIANA NA MAKUNDI
MBALIMBALI ILI KUTOA TAALUMA JUU YA UMUHIMU WA MAHKAMA HIYO ILI IWEZE
KUFANYA KAZI ZAKE KWA UFANISI.
JUMLA YA DOLA ZA KIMAREKANI ELFU TANO ZIMETUMIKA KATIKA UJENZI WA MAHAKAMA HIYO KWA UFADHILI WA SWEDEN .
No comments:
Post a Comment