Wapinzani wa rais wa Misri wameitisha
maandamano zaidi , wiki moja baada ya ghasia ambazo zilisababisha mauaji
mengi zaidi tangu rais Morsi achukue mamlaka mwaka jana.
Zaidi ya watu sitini wameuawa . Jana wanasiasa
waliafikiana kwa kauli moja kulaani ghasia na kufanya mazungumzo kama
njia ya kumaliza mzozo unaoikumba nchi hiyo.Lakini mazungumzo yao yalikaribia kukatizwa pale makundi ya vijana yalipotoa wito wa kufanyika kwa maandamano zaidi dhidi ya rais Mohamed Mosri baada ya sala ya ijumaa.
Walimshutumu kiongozi huyo wa kiislam kwa kulazimisha mageuzi mapya ya kiimla na kukiuka malengo ya mapinduzi yao ya miaka miwili iliyopita .
Kuna mipango ya waandamanaji kukusanyika katika medani ya Tahrir ambapo wanatazamiwa kuandamana hadi kwenye makao ya Rais.
Wafuasi wa bwana Morsi wanasema ni njama ya kutumia nguvu ya maandamano ya mtaani kuuangusha utawala wa kwanza uliochaguliwa wa kidemokrasia nchini Misri
No comments:
Post a Comment