7 Februari, 2013 - Saa 07:58 GMT

Inaarifgiwa polisi mmoja aliuawa kwenye maandamano hayo
Kumekuwa na utulivu mjini Tunis,
Tunisia usiku kucha baada ya siku moja ya vurugu kufuatia mauaji ya
mwanasiasa mashuhuri wa upinzani Shokri Belaid.
Waziri Mkuu wa Tunisia, Hamadi Jebali, amesema ataunda Serikali ya watalamu kufuatia mauaji ya Belaid.Lakini mmoja wa viongozi wa serikali alilaani mauaji hayo akiyataja kuwa kitendo cha uoga na kuwa wale waliomuua kiongozi huyo hawatafanikiwa kusababisha vurugu Tunisia.
Mauaji ya Bwana Belaidi, ambaye amekuwa mkosoaji mkuu wa Serikali yalisababaisha ghasia katika miji kadhaa nchini. Waandishi wa habari kutoka eneo hilo wanasema kufikia sasa afisaa mmoja wa polisi ameuliwa na waandamanaji hao.

Jamaa za marafiki za marehemu Shokri Belaid
Maelfu ya waandamanaji walikuwa wametoa wito kujiuzulu kwa chama kinachotawala cha Kiislamu cha ENNAHDA kufuatia mauaji ya Belaid.
Muungano wa vyama vya kiraia uliokuwa mwanachama wa serikali ya muungano, uliondoka Serikalini na kuitisha mgomo wa taifa lote.
No comments:
Post a Comment