Miili minne mingine imegunduliwa kichakani baada ya uvamizi katika kijiji cha Kaptir nchini Kenya siku ya Ijumaa, kufikisha idadi ya vifo kufikia 10, gazeti la The Standard la Kenya liliripoti siku ya Jumamosi (tarehe 9 Februari). .
Familia za wachungaji zimeanza kuhama kutoka eneo hilo bada ya
mashambulizi ya Ijumaa, ambapo mifugo 2,000 iliibwa, afisa mkuu wa
Turkana ya Kusini John Bosco Muutu alisema.
"Wamehama kuepuka kufikiwa na uvamizi mwengine," alisema. "Lakini
tumezidisha usalama katika eneo hilo ili kuzuwia mashambulizi zaidi."
Miongoni mwa waliouawa ni askari wa akiba, wakati watu wengine watatu
wanashukiwa kuwa wanatoka upande wa uvamizi, Muutu alisema.
Polisi wanashuku kuwa baadhi ya wavamizi walikimbilia Uganda na
wanyama walichukuliwa kuelekea Pokot ya Kaskazini, alisema Mkuu wa
Wilaya ya Turkana ya Kusini Elijah Kodoh. "Tumewaomba wenzetu walioko
Pokot ya Magharibi na Kaskazini kushiririkiana ili kuwapata wanyama
walioibwa," alisema.
Eneo la Turkana hivi karibuni limeshuhudia uvamizi wa mifugo, ikiwa
ni pamoja na shambulizi katika jimbo la Baringo wiki iliyopita ambapo majambazi waliwapiga risasi na kuwaua watu sita, wakiwemo maafisa wa polisi watatu.
No comments:
Post a Comment