Friday, February 1, 2013
WAPIGA DEBE JANGOMBE MAGENGENI WAWAPA HOFU KUBWA WANANCHI
Imewekwa na Hamed Mazrouy
Wananchi wa Shehi ya Jangombe Gengeni wamelalamikia kuzidi kwa matendo maovu ndani ya shehia yao yanayofanywa na wapiga debe wa gari za abiria kwenye kituo cha daladala kilichopo maeneo hayo.
Wakizungumzia na Mwandishi wetu huko Jangombe baadhi ya Abiria wanaotumia kituo hicho cha Daladala kwa masharti ya kutotajwa majina waesema kuwa wamekuwa na gamu kubwa sana wanapotaka kushula au kupanda Daladala maeneo hayo kutokana na kushamiri kwa kiasi kikubwa sana matendo maovu yanayofanywa na wapiga debe hao.
Wakibainisha baadhi ya matendo wanayoyafanya wamesema kuwa ni kunyanganywa mizigo yao wanayokuwa nayo tena kwa kutumia nguvu wakati mwengine huwatishia mpaka na silaha jambo ambalo si sheria waka hapaswi kufanyiwa mtu yoyote yule kwa mujibu wa sheria za nchi hii.
Wananchi hao wamendelea kufahamisha kuwa wanashanhagazwa na wahusika kutokuwadhiti wanaofanya matendo hayo kwani wanawajua na kuwaona licha ya kuwepo kituo kidogo cha Pilisi maeneo ya karibu na hapo.
Aidha waliliomba Jeshi la Polisi kutoa ushirikiano wa hali ya ju kuhakikisha kuwa eneo hilo lipo salama na wananchi wanalitumia kwa shuughuli zao bila ya usumbufu uliopo sasa.
kwa msaada wa habari za mawio.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment