
Ni ukweli usiofichika kuwa moja miongoni mwa nyenzo muhimu za maendeleo ni kuwepo kwa mawasiliano ya barabara kwani huweza kuwarahisishia jamii husika kupata mawasiliano kwa muda mfupi.
Zaidi ya shillingi bilioni tano zimetengwa kutumika kwa ajili ya matengenezo ya barabara za Unguja na Pemba katika kipindi cha mwaka huu.
Mkurugenzi
wa idara ya ujenzi na utunzaji barabara zanzibar Bw Ali Twahir Fatawi
amesema kuwa fadha hizo zitatumika kukamilisha ujenzi wa barabara ya
amani mtoni yenye urefu wa kilomita nne na barabara ishirini za ndani
Unguja na Pemba
Ameyasema
hayo wakati akizungumza na mwandishi wetu katika ujenzi huo utaweza
kuhusisha utiaji wa lami, kifusi pamoja na matengenezo mengine kwenye
barabara mbali mbali zilizopo Zanzibar.
Bw
fatawi akizungumzia kuhusu suala la utunzaji wa barabara inashirikiana
na vikundi vya kijamii kuweka mipango ya uhifadhi wa barabara ili
zidumu kwa muda mrefu.
No comments:
Post a Comment