
Amesema kutokana na hali hiyo kunahaja ya kuwalinda watoto hao ambao ni tegemeo la maendeleo ya taifa la baadae.
Akizindua
huduma ya chanjo ya ugonjwa wa kuhariha, nemonia na uti wa mgongo
inayotolewa kwa watoto chini ya mika mitano mhe duni amesema huduma hiyo
iliyoanza kutolewa kwa wiki tatu sasa itasaidia kupunguza maradhi
hayo ambayo ni hatari kwa watoto.
Mh
juma duni amewasisitiza wazazi kushirikiana na watendaji wa sekta ya
afya ili kuhakikisha watoto wao wanapatiwa chanjo kwa wakati.
Nae mratibu wa chanjo za Mama na watoto zanzibar bw Yussuf Haji Makame amesema jamii imekuwa na uelewa mkubwa juu ya kinga mbalimbali zinazotolewa kwa watoto na wamejiepusha katika imani za potofu.
Amesema
chanjo hizo za ugonjwa wa kuhariha, nemonia na uti wa mgongo
zitatolewa kwa awamu mbili kwa watoto wenye umri kuanzia wiki sita
hadi wiki kumi.
No comments:
Post a Comment