4 Machi, 2013 - Saa 08:05 GMT

Mido Macia akiburuzwa nyuma ya gari la polisi
Polisi wanane wa Afrika Kusini
wanategemewa kufikishwa mbele ya mahakama kuhusiana na kisa cha wiki
iliyopita ambapo mtu mmoja, raia wa Msumbiji, aliburuzwa nyuma ya gari
la polisi.
Mido Macia, 27, alifariki kutokana na majeruhi
aliyopata kichwani na alipovuja damu mwilini, baada ya kukamatwa huko
Daveyton, mashariki mwa Johannesburg.Rais Jacob Zuma alisema tukio hilo lilikuwa "baya sana" na "lisilokubalika".
Maafisa hao Ijumaa iliyopita walifunguliwa mashataka ya mauaji, siku tatu baada ya tukio hilo.
Bwana Macia, dereva wa magari madogo ya abiria, alikamtawa kwa madai ya kuegesha gari lake mahala ambapo alizuia magari mengine
No comments:
Post a Comment