4 Machi, 2013 - Saa 05:11 GMT

Makadinali wa Kikatoliki
Makadinali wa Kanisa
Katoliki kutoka kote duniani wamekusanyika mjini Roma kuanza mkutano wa
awali wa faragha wa kumchagua mrithi wa Papa Benedict XVI.
Mkutano huo utaamua tarehe ya kuanza utaratibu
wa mfululizo wa kura za siri. Makadinali hao watafanya mikutano ya kila
siku hadi hapo papa mpya atachaguliwa.Wahandisi wa ufundi wa teknolojia ya mawasiliano watakuwa wakiwachunguza makadinali, na simu zao zitapigwa marufuku wakati wa shughuli hiyo.
Uchaguzi huu unfanywa baada ya Papa Benedict XVI kujiuzulu baada ya miaka minane ya kuwaongoza Wakatoliki bilioni 1.2.
Ni papa wa kwanza kujiuzulu katika miaka 600
No comments:
Post a Comment