Thursday, March 28, 2013

Uhuru wa mavazi Tunisia waleta hofu

 28 Machi, 2013 - Saa 13:01 GMT
Wanawake wa Tunisia wakitaka haki zao
Miaka miwili baada ya kupinduliwa utawala wa muda mrefu Tunisia, wanawake nchini humo wanafurahia uhuru wao wa kuvaa nguo kama vile Niqab, vazi linaloufunika uso mzima wa mwanamke, huku wengine wakiwa na hofu ya kupoteza uhuru wao.
Huku chama chenye itikadi kali za dini ya kiislamu kikiwa na uwakilishi mkubwa bungeni, sera zisizo za dini za utawala uliokuwpeo zimeondolewa huku wanaume zaidi wakiamua kufuga ndevu na wanawake wengi kuvaa mabaibui nchini Tunisia.

Hili ni jambo linalowatia wasiwasi baadhi ya wanawake.

Katika maandamano ya hivi karibuni watu 800 walimiminika katika eneo la Habib Bourguiba katikati mwa mji wa Tunis, wakiimba kutaka kuwa na taifa lisilo la kidini na kukipinga chama cha Muslim Brotherhood.
Chini ya utawala wa Zine el-Abidine Ben Ali, wanawake wa Tunisia walikuwa na uhuru zaidi kuliko wanawake wengine katika ulimwengu wa kiarabu.
Wanaweza kuwawacha waume zao kwa misingi sawa kama waume na ndoa za mke zaidi ya mmoja zimepigwa marufuku, ambapo katika nchi nyingi za kiislamu mwanamume anaruhusiwa kuoa mke zaidi ya mmoja, licha ya kwamba kwa mujibu wa sheria wanaume wanastahili sehemu kubwa ya urathi.
Hali kwa wanawake wa Tunisia sasa, miaka miwili tangu kuangushwa utawala nchini humo ni ya kuchangayika.
Amna Guellali anayefanya kazi na shirika la kimataifa la kutetea haki za kibinadamu nchini Tunisia anasema serikali mpya, iliyo na idadi kubwa ya wanachama wa chama chenye itikadi kali za dini ya kiislamu Ennahda.
Wengi wanapinga utawala wa kiisilamu wakisema wanataka uhuru zaidi
Said Ferjani, ambaye ni mwanachama mkuu wa chama hicho anasema hawanuii kushinikiza namna ya kuishi miongoni mwa watu ila lengo lao ni kutetea uhuru.
Chama hicho kiliondoka madarakani baada ya makabiliano kuhusu maneno yanayotumika katika katiba mpya, maandiko katika rasimu yalitaja haki kati ya wanaume na wanawake kulingana hali inayoambatana na maadili ya chama cha Ennahda, lakini baada ya malalamiko kutoka makundi ya wanawake neno kulingana lilibadilishwa na kuwa usawa.
Wanawake wengi Tunisia wanaona haki zao zinatishiwa.
Tunisia inasalia kuwa huru ikilinganishwa nchi nyengine jirani, wanwake wengi hawajifuniki na hata pia ma shekhe na maafisa wa chama cha Ennahda huwaamkua wanawake kwa kuwapa mkono.
Lakini watu wengi wanaamua kuvaa baibui ambalo lilipigwa marufuku chini ya utawala uliokuwepo.
Ni jambo la kawaida sasa kuwaona wanaume wakifuga ndevu, wakivaa kofia na kanzu za msikitini. Mavazi ya wahafidhina wa dini ya kiislamu.
Baadhi ya wanawake wanalalamika kushinikizwa kuvaa baibui, huku vijana wakieleza kwamba wanalazimishwa na wahafidhina kuacha kulewa na kucheza kamari.
Kuna wanaoona haya kama thibitisho la ushawishi wa mataifa ya nje hususan kutoka nchi kama Saudia na Qatar.
Lakini kwa raia wa Tunisia wenye itikadi kali za dini ya kiislamu ni hatua ya kuidhinisha upya wazi kitambulisho chao cha kiislamu na kiarabu baada ya kudhalilishwa kwa miaka mingi na utawala wa Ben Ali na Habib Bourguiba.

No comments:

Post a Comment