Tuesday, March 26, 2013

Eurozone yaziokoa benki za Cyprus

 25 Machi, 2013 - Saa 07:02 GMT
Wateja wapiga foleni ili kutoa pesa
Wateja wapiga foleni ili kutoa pesa
Mawaziri wa fedha wa Eurozone wamekubali kuipa Cyprus mkopo wa euro bilioni 10 ili kuzuia mfumo wake wa benki usiangamie, na pia kuhakikisha kwamba nchi hiyo inabaki katika eneo la eurozone.
Benki ya Laiki – benki ya pili kwa ukubwa nchini – itafungwa taratibu. Wateja watakaoathirika zaidi ni wale waliohifadhi zaidi ya euro 100,000, amabo yasemekama watakatwa fedha fulani.
Lakini wateja wa benki wenye chini ya euro 100,000 euros, fedha zao "zitalindwa".
Kamishna wa Masuala ya Kiuchumi ya EU, Olli Rehn, amesema kwamba "kina cha matatizo ya kifedha nchini Cyprus chamaansisha kwamba hali ya baadaye itakuwa ya shida kwa nchi hiyo na watu wake".
Nalo Benki la Cyprus – benki kubwa kabisa kisiwani humo – Jumapili iliwakubalia wateja watoe kiasi cha euro 120 kwa siku tu toka mashine za kutolea pesa za ATM.
Foleni ndefu zilionekana za watu wakitoa pesa. Benki zimefungwa tangu Jumatatu iliyopita.

No comments:

Post a Comment