27 Aprili, 2013 - Saa 14:47 GMT
Polisi wa Bangladesh wanasema
kuwa wamewakamata wahandisi wawili ambao inasemekana walihusika na jengo
la kiwanda liloporomoka mjini Dhaka siku ya Jumatano na kuuwa watu
zaidi ya 300.
Tajiri wa viwanda vya kutengenza nguo kwenye jengo hilo pamoja na meneja wake mkuu piya wamekamatwa.
Watu wanaofanya kazi za uokozi bado wanafukua kifusi kujaribu kuwafikia mamia ya watu ambao wanafikiriwa kuwa bado wamenasa.
Watu kama 26 walinusuriwa Jumamosi huku waokozi wamekuwa wakipenyeza chakula na maji kwa manusuru walionasa ndani ya kifusi.
No comments:
Post a Comment