Sunday, April 28, 2013

Sri Lanka haifai kuandaa Commonwealth

 27 Aprili, 2013 - Saa 15:48 GMT


Canada imeeleza kuwa ni jambo la kuchusha sana kuwa Sri Lanka itaruhusiwa kuandaa mkutano wa viongozi wa nchi za Jumuia ya Madola baadae mwaka huu.
Waziri wa  mambo ya nchi za nje wa Canada, John Baird
Waziri wa Mashauri ya Nchi za Nje wa Canada, John Baird, aliiambia BBC kwamba msingi wa jumuiya ya Commonwealth ni kuhusu maadili kama ya kufuata sheria, demokrasia na utawala bora.
Alisema serikali ya Sri Lanka haikuheshimu hayo.
Alisema kuna ushahidi mzito na unaozidi kwamba ulitokea uhalifu wa kivita mwisho wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Sri Lanka, na serikali haikufanya juhudi za kutosha kupatana na jamii ya kabila la Tamil.
Serikali ya Sri Lanka imeagiza uchunguzi wake yenyewe kuhusu tuhuma za uhalifu wa kivita.

No comments:

Post a Comment