30 Aprili, 2013 - Saa 07:23 GMT
Uingereza imetangaza kuwa itakoma kutoa msaada kwa Afrika Kusini kuanzia mwaka 2015.
Waziri wa maendeleo ya kimataifa, Justine
Greening, anatarajiwa kutangaza rasmi hatua hiyo itakayoinyima afrika
kusini msaada wa moja kwa moja wa dola milioni thelathini kila mwaka
baadaye hivi leo.Maafisa wanasema hatua hiyo ni ya kutambua ustawi wa Afrika kusini tangu kukamilika kwa utawala wa kibaguzi, huku taifa hilo likionekana kuwa na uwezo wa kutoa msaada kwa mataifa mengine.
Katika hatua kama hiyo Uingereza ilisitisha kutoa msaada kwa taifa la India mwaka uliopita.
No comments:
Post a Comment