Kwa mujibu wa Taasisi ya Utafiti ya Wanyamampori Tanzania, ujangili umepunguza kwa kiasi kikubwa jamii ya tembo kuwa wachache kuliko 70,000 mwaka 2012 kutoka kwenye kiasi takribani 109,000 mwaka 2009.
Hasira miongoni mwa watunga sheria kuhusu kuongezeka kwa ujangili, Waziri wa Maliasili na Utalii Khamis Sued Kagasheki aliliambia bunge Alhamisi (tarehe 2 Mei) kwamba rais Kikwete aliidhinisha kusambazwa kwa vikosi vya jeshi kwa ajili ya operesheni dhidi ya ujangili.
"Rais alitoa agizo," Kagasheki aliliambia bunge. "Nimezungumza na waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa [Shamsi Vuai Nahodha] na tuko katika hatua za mwisho. Sisemi ni lini, lakini tutafanya kitu ambacho kitakumbukwa na kizazi kijacho."
Hii ni mara ya pili kwa jeshi kusaidia dhidi ya ujangili, Mwaka 1989, "Operesheni Uhai" ilisaidia jamii ya tembo kuongezeka tena baada ya kupungua hadi kufikia 30,000, ambapo walikuwa takribani 110,000 mwaka 1976.
Wabunge wapokea kwa furaha uamuzi
Mbunge wa upinzani Peter Msigwa alisema anaunga mkono uamuzi wa rais kupeleka vikosi kupambana na majangili, lakini alisema serikali ilipaswa kuwa imechukua hatua hii miaka mitano iliyopita."Mwaka 2008, tatizo la ujangili lilikuwa kubwa kama ilivyo sasa," aliiambia Sabahi. "Kilio cha wananchi kusambaza jeshi kilikuwa kikubwa, lakini serikali haikutaka kutusikiliza."
Nchi zinapaswa kuungana kusimamisha biashara hii haramu kidunia ya "pembe za ndovu", alisema, kwani biashara hii haramu inakua kwa haraka kwa gharama ya maliasili za Tanzania.
Kabla ya bunge Ijumaa, Gosbert Blandes, mbunge anayewakilisha jimbo la Karagwe, alisema operesheni ya jeshi iliyopendekezwa inapaswa kuanza mara moja.
"Ninataka waziri aseme sasa hivi ni lini operesheni hii inaanza? Nini tunachoficha? Inapaswa kuanza mara moja na si kinyume chake," alisema.
Kagasheki alikataa kutoa maelezo zaidi kuhusu mipango ya jeshi, akisema kwamba kufichua maelezo yote kunaweza kuishia kuwasaidia majangili. Hata hivyo, alisema inaweza kuanza "hivi karibuni" na kwamba safari hii wanajeshi wanaweza kutumia vifaa vya kisasa ili kusaidia kuwavamia majangili.
Kiongozi wa upinzani Freeman Mbowe alisema aliridhishwa na kusudi la serikali kutumia jeshi kukabiliana na ujangili, lakini alisema serikali inapaswa kuongeza jitihada.
"Kama hatua za kuzuia, tunapaswa kubadilisha sheria zetu ili zieleze wazi kwamba yeyote atakayekamatwa akijihusisha na ujangili anapaswa kuhukumiwa kifo," aliiambia Sabahi.
Mashambulizi kufuatilia mbuga za wanyama
Msemaji wa Mbuga za Wanyama Tanzania Pascal Shelutete alisema huduma za mbuga zitatumia mashambulizi -- ndege ndogo zisizokuwa na marubani, zinazodhibitiwa kwa mbali na zenye kamera -- kufuatilia nani anayeingia mbugani."Ni aina ya kamera zilizoboreshwa za televisheni, ambazo zitawezesha ufuatiliaji katika mbuga zote kwa saa 24," Shelutete aliiambia Sabahi, akiongeza kwamba kamera zimeunganishwa katika kompyuta kupitia satelaiti.
Miradi kama hiyo imefanyika duniani kote. Mfuko wa Hifadhi ya Wanyamapori Duniani una kundi la ndege zisizokuwa na marubani, ambazo zimewasaidia kuhifadhi tembo, faru na chui wa Nepali.
Aidha, miradi katika hifadhi nyingine za wanyamapori za Afrika imetolewa na Mfuko wa Kimataifa wa Kuzuia Ujangili (IAPF), ambayo inasaidia mfuko katika upatikanaji wa washambuliaji kwa ajili ya jitihada za hifadhi.
"Tunapigana vita dhidi ya majangili wenye silaha na waliojiandaa vya kutosha," IAPF ilieleza katika tovuti yake. "Katika muktadha wa kupunguza ujangili katika mazingira hatari, [ndege zisizokuwa na marubani] zinaweza kufika sehemu pana, kwa usalama zaidi na kuleta suluhisho la gharama nafuu, na kuwaruhusu waangalizi wa mbuga kufuatilia eneo kubwa zaidi la ardhi huku wakipunguza kuonekana kwao kwa majangili hatari na wenye silaha."
Naibu waziri wa Maliasili na Utalii Tanzania Lazaro Nyalandu aliwaomba wananchi kuunga mkono jitihada dhidi ya majangili kwa kutoa taarifa katika mamlaka zinazohusika kwa kitu chochote watakachoona au kusikia kikihisishwa na ujangili.
"Serikali haiwezi kupigana vita ya ujangili ikiwa peke yake. Tunatakiwa kushirikiana kama Watanzania kupambana na majangili kama njia ya kutunza maliasili zetu," alisema akilihutubia bunge siku ya Ijumaa. "Tujengeni tabia ya kuripoti kitu chochote tunachoona kinahatarisha tembo wetu, faru na maliasili nyingine zote."
No comments:
Post a Comment