Aliyekuwa kiongozi wa vugu vugu
la vijana la chama tawala nchini Afrika Kusini cha ANC, Julius Malema
amezindua kundi la kisiasa litakalojulikana kama Wapiganiaji wa Uhuru wa
Kiuchumi au Economic Freedom Fighters, EFF.
Malema, ambaye alitimuliwa kutoka kwa chama cha
ANC, mwaka wa 2012, amesema chama chake cha EFF kinataka zoezi la
kugawanya mashamba kuanzisha upya na pia kutaifishwa kwa migodi yote ya
madini.''Tutagawana ardhi sisi zote ukiwa mweusi au mweupe. Lakini ukikataa kugawanya itamaanisha kuwa utalazimishwa kufanya hivyo'' Alisema Bwana Malema.
Ametaja dhamira kuu ya vugu vugu hilo kuwa kupamabana mfumo wa kipebari.
Akiwa amevalia kofia nyekundu iliyo na maandishi ''Amirijeshi Mkuu wa EFF'' Bwana Malema amewaambia waandishi wa habari kuwa chama chake kimebuniwa ili kutetea maslahi ya raia wanaoteseka katika maeneo ya mashinani.
EFF kukupambana na ANC katika uchaguzi mkuu
Malema ameshutumu rais Zuma kwa kutoimarisha juhudi za kuwasaidia raia weusi wa nchi hiyo ambao ni masikini na waliompigia kura.
Hata hivyo haijabainika ikiwa atawania kiti chochote katika uchaguzi mkuu utakaoandaliwa mwaka ujao, akisema kuwa uamuzi huo utatolewa baada ya mkutano wa baraza kuu la chama hicho cha EFF utakaofanyika mwisho wa mwezi huu.
Wachanganuzi wa kisiasa wanasema idadi kubwa ya raia wa Afrika Kusini, wamepoteza imani na chama cha ANC, ambacho kimekuwa madarakani tangu mwaka wa 1994.
Rais wanasema maafisa wengi wa chama hicho ni wafisadi na hawana nia ya kuimarisha hali ya maisha.
No comments:
Post a Comment