Serikali ya Nigeria imesitisha
mpango wake wa kuzuia mawasiliano ya simu katika jimbo moja kati ya
majimbo matatu ambayo hali ya hatari imetangazwa kwa sababu ya
mashambulio ya mara kwa mara kutoka kwa wanamgambo.
Jimbo la Adamawa halijaadhiriwa pakubwa na mashambulio hayo yanayofanywa na wapiganaji wa Kiislamu wa Boko Haram.Wiki iliyopita, afisa mmoja mwandamizi wa serikali alisema kuwa ukosefu wa mawasiliano ya simu, ulizuia raia kutoa habari kwa serikali wakati shule moja ilipovamiwa.
Lakini jeshi la nchi hiyo limesema, uamuzi huo ulichukuliwa ili kuzuia wanamgambo hao kupanga mashabulio hayo.
Kundi la Boko Haram linadaiwa kuwaua zaidi ya watu elfu mbili tangu ilipoanzisha mashambulio yake mwaka wa 2009.
Wizara ya Ulinzi nchini Nigeria, limesema hali ya ulinzi imeimarika katika jimbo hilo la Adamawa.
Mwandishio wa BBC nchini Nigeria, alifanikiwa kuwasiliana na mkaazi mmoja wa jimbo hilo la Adamawa mapema siku ya Ijumaa.
Hata hivyo mawasiliano katika majimbo jirani ya Yobe na Borno bado yamekatizwa.
Mwezi Juni mwaka huu jeshi la nchi hiyo lilitangaza kuwa mtu yeyote atakayepatikana na simu ya Satellite katika jimbo la Borno atakamatwa.
Gavana huyo hata hivyo alitoa wito kwa serikali kurejesha mawasiliano ya simu ili kusaidia raia kutoa habari kwa utawala wakati kunapotokea mashambulio.
Mawasiliano ya simu za nyaya nchini Nigeria mara nyingi hazifanyi kazi nje ya miji mikuu ya Abuja na Lagos.
Wanajeshi zaidi wametumwa katika majimbo ya Kaskazini mwa Nigeria tangu serikali ilipotangaza hali ya tahadhari.
Kundi la Boko Haram, ambalo majina yake yanamaanisha Elimu ya mataifa ya Magharibi hairuhusiwa, inataka sheria za Kiislamu kutumika katika eneo la Kaskazini lenye idadi kubwa ya waumini wa dini ya Kiislamu.
No comments:
Post a Comment