Tuesday, December 4, 2012
JESHI LA POLISI LAWATAKA WANANCHI KTOKUWATUPIA LAWAMA ZISIZO ZA MSINGI.
Kaimu mkuu wa upelelezi mkoa wa mjini magharib nd:Haji A Hji ametoa wito kwa jamii kuwacha kutupishia lawama jeshi la polisi dhidi ya makosa ambayo yanasababishwa na wananchi wenye,hali ambayo inasababisha jeshi hilo kuonekana kua hali tendi haki katika kesi hizo. Hayo ameyaeleza huko ofisini kwake madema wilaya ya mjini wakati alipokua akizungumza na waandishi wa habari dhidi ya tuhuma kali zilizo iandama jehi la polisi kuwa hawatendi hakika kesi zinazo letwa na wanachi kutoka sehemu tofauti. Kaimu huyo amewataka wananchi waache kulalamika ovyo kwa kesi ambazo wanazisababishwa wao wenyewe,ambazo wanazifikisha kituoni bila ya ushahidi halisi jambo ambalo linawawiya vigimu jeshi hilo kumshikilia mtuhumiwa ambae hakuna uhakika wa kosa lake.
Pia aliendelea kufahamisha,kuwa baadhi ya walio wengi wanafahamu kua,mtuhumiwa yoyote ambae amepelekwa kituoni ni lazima kwake kuhukumia kifungo bali sivyo ni lazima kuwe na ushahidi wa hakika kutokana na kesi yake,lakini walio wengi badala ya kumfikisha mtuhumiwa hua hawapiti tena na baadae kulilaumu jeshi la polisi.
Nd:Haji amesema,tatizo kubwa ambalo lina wakumba ni pale wananchi wanapo mfikisha mtuhumiwa polisi na baadae kupatana wao kwa wao na hatimae jeshi kukosa ushahidi,jambo ambalo linawafanya kutokua na uamuzi wa kumuhukumu na badala yake kumwachilia huru.
Hivyo Mkuu huyo amewataka wananchi kwa ujumla wanapo mfikisha kituoni mtuhumiwa pia wawe tayari kutoa ushahi na kuisimamia kesi hiyo hadi kufikia mwisho badala ya kuwaleta tu na kutojitokeza katika ushahidi,na wanapo achiliwa kulipashutma jeshi hilo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment