Watu kumi na tisa walikufa karibu na mji wa Molo nchini Kenya pale
basi dogo la abiria 14 lililobeba kiasi cha watu 28 lililokiuka barabara
na kuingia kwenye mtaro siku ya Jumatano (tarehe 2 Januari), liliripoti
gazeti la The Standard la Kenya.
Watu kumi na saba, akiwemo dereva, walikufa hapo hapo, huku wawili
walikufa kutokana na majeraha baadaye katika Hospitali ya Wilaya ya
Molo.
Gari hilo ilikuwa imepakia kupindukia na ilikuwa ikienda kwa kasi
wakati ilipoacha barabara, alisema Mkuu wa Polisi wa Bonde la Ufa, John
Mbijiwe, aliyeonya kwamba ikiwa kuna polisi yeyote aliyekuwa ameiona
matatu hiyo na hakuchukua hatua atawajibishwa.
“Halikubaliki kuona Wakenya wasio hatia wakipoteza maisha yao wakati tayari sheria mpya za barabarani zipo,” alisema.
Ajali hiyo imetokea siku moja tu baada ya watu 11 kufa kwenye ajali
nyengine ya gari katika barabara kuu ya Nakuru-Eldoret. Kwa uchache watu
54 wamekufa nchini Kenya katika ajali za barabarani tangu tarehe 31
Disemba, kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation la Kenya.
No comments:
Post a Comment