Polisi wa Somalia na vikosi vya Umoja wa Afrika nchini humo vimeanza
doria za usiku mjini Mogadishu, uliripoti mtandao wa al-Shahid wa
Somalia siku ya Jumatano (tarehe 2 Januari).
Doria hizo zinakusudiwa kuweka usalama wa jumla na zitaendelea hadi
Mogadishu iwe salama, alisema Jenerali Abdullahi Hassan Barise, mkuu wa
upelelezi wa makosa ya uhalifu katika Kikosi cha Polisi ya Somalia.
Doria hizo mpya za usiku zinafuatia tangazo la Waziri Mkuu Abdi Farah
Shirdon mnamo tarehe 29 Disemba kwamba serikali ya Somalia imewapa
mafunzo wanajeshi 1,000 kuchukua nafasi na kuzuia kurudi kwa vizuizi haramu vya barabarani mjini Mogadishu.
No comments:
Post a Comment