Rais
wa Zanzibar na Mweenyekiti wa Barza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed
amesema Uzinduzi wa Mradi wa Serikali Mtandao E-Government umefungua
ukurasa mpya katika uendeshaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na
utekelezwaji wake utaakisi lengo kuu la Mapinduzi ya Zanzibar la
kuwakomboa Wananchi kimawazo na kiuchumi.
Rais
Shein ameyasema hayo katika hotuba yake ya uzinduzi wa Mradi huo
iliyofanyika Mazizini nje kidogo ya mji wa Zanzibar ikiwa ni shamra
shamra za miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar
Amesema
lengo la Mradi wa E-Government ni kuiwezesha Serikali kuendesha shughuli
zake kwa njia za kitaalamu zaidi na kuhakikisha kuwa kila mwananchi
popote alipo anapata huduma au taarifa muhimu zinazotolewa na Serikali
kupitia mitandao mbalimbali itakayokuwa karibu naye.Ameongeza kuwa Mradi huo utaisaidia sana Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kufanya kazi zake kwa ufanisi mkubwa na kwa haraka katika kukabiliana na kasi ya mabadiliko ya kilimwengu kama yanavyoshamiri siku hadi siku duniani.
“Ni jambo la fahari sana kuwa leo hii Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inajiunga rasmi na nchi zingine duniani katika mfumo mpya wa uendeshaji wa shughuli za kiserikali ujulikanao kama E-Government” alisema Shein.
Ameongeza
kuwa Mradi huo pia utakuwa ni kichocheo muhimu katika kuendeleza
dhamira ya Serikali ya kukuza matumizi ya Teknologia ya habari na
Mawasilino nchini.
Amezitaja
baadhi ya faida za Serikali Mtandao kuwa ni pamoja na kukuza Elimu
katika Skuli za Msingi na Sekondari kwa kupitia Mradi wa T21, ili
kukabiliana na mabadiliko yanayoikumba sekta ya habari na mawasiliano.
Aidha
Dkt. Shein amefahamisha kuwa Mradi huo pia unaweza kuipunguzia gharama
Serikali ya kusafirisha wagonjwa nje ya nchi kwa matibabu ambapo
Madaktari wa ndani wanaweza kuunganishwa na madaktaari waliopo nje ya
nchi na kuweza kusaidiana kuwafanyia Operesheni wagonjwa waliopo
Zanzibar.Dkt Shein pia amefahamisha kuwa Mradi huo utatoa fursa nzuri kwa wafanyabiashara na wawekezaji nchini katika kundesha biashara zao ikiwa ni pamoja na kujtangaza,kutafuta masoko na kutoa huduma bora kwa wateja wao.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais utumishi wa Umma na Utawala Bora Haji Omar Kheri amesema Taasisi za Kiserikali zitaunganishwa katika utendaji na uendeshaji wa shughuli zao kwa njia za uhakika,salama na kwa uharaka.
Aidha amewataka wananchi kuiheshimu miundombinu ya mradi huo ili uweze kuwa endelevu kwa manaufaa ya wananchi wote.
Akitoa
salam zake Balozi wa Watu wa China nchini Tanzania Lu Youqing
ameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mashirikiano ambayo
imekuwa ikitoa kwa nchi ya China katika kuendeleza mahusiano ya nchi
husika.
Aidha
ameahidi kuzidisha mashirikiano na Zanzibar katika kusaidia wananchi
wake kukabiliana na changamoto za maisha hasa katika sekta ya
uchumi,elimu na Afya.
Mradi
wa Serikali mtandao E-Government ambao umezinduliwa ikiwa ni shamra
shamra za Sherehe za miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar umeigharimu Dola
Milion 19 za kimarekani ambazo ni Mkopo nafuu kutoka nchi ya China.
No comments:
Post a Comment