MAKAMU wa Kwaza wa rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, ameuagiza uongozi wa Skuli mpya ya Sekondari ya ‘Dk Omar Ali Juma’ kuanzisha kamati maalum za utunzaji wa skuli hiyo, ili iweze kuwa endelevu na kudumu kwa muda mrefu.
Alisema, imekuwa ni kawaida mara majengo kama hayo yanapokabidhiwa kwa taasisi husika, kukaa bila ya kushughulikiwa, hivyo kwa skuli hiyo na jina iliopewa, ni vyema suala la matunzo likapewa umuhimu wa pekee.
Makamu
huyo wa Kwanza wa rais wa Zanzibar , aliyaeleza hayo jana huko Skuli ya
Wawi Wilaya ya Chake chake Pemba , mara baada ya kuifungua skuli hiyo
ya ‘Dk Omar Ali Juma’ yenye vyumba kumi na mbili, vitatu vya maabara na
ukumbi wa mkutano ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya miaka 49 ya
Mapinduzi Zanzibar
Alisema
kuwa jina la Dk. Omra Ali Juma, ni kubwa katika taifa hili, hivyo haiwi
busara skuli hiyo baada ya mwaka ikaanza kuchakaa na kupoteza haiba na
uzuri wake, jambo ambalo halitoleta sura nzuri kwa wenyeji na wageni.
Alisema
ni vyema uongozi wa skuli hiyo kwa kushirikiana na kamati ya Skuli,
uongozi wa shehia za Wawi na Mgogoni na wananchi wote, kukaa pamoja ili
kuweka mikakati ya kuilinda skuli hiyo kwa maslahi yao na kizazi
kijacho.
‘’Kabla
ya uzio mlioombwa kujengwa ili kuizungurishia skuli hii haujaja, ni
vyema kwanza mkakaa pamoja na kuona mnafanya nini katika kuilinda skuli
hiyo na kuitunza hasa kwa vile mamilioni ya fedha yametumika’’, alieleza
Maalim Seif.
Aidha
amesema, kwa vile wafugaji wa shehia za Wawi na Mgogoni wanajulikana,
na uongozi wa shehia upo, kusiwe na sababu ya mfugaji atakaefunga
Ng’ombe wake katika eneo hilo kuonelewa haya kwa vile anaharaibu mali ya
umma.
Makamau
huyo Kwanza alizidi kueleza kuwa, hadhi ya jengo hilo pamoja na vifaa
vilivyomo ndani yake, haiwi busara kuanza kuliacha bila ya kulitunza
hasa kwa vile wanaotarajiwa kufaidika kwanza, ni vijana wa Wawi na
Mgogoni.
Akizungumzia
kuhusu elimu, aliwataka wazazi na walezi kuendelea kujenga ‘utatu’ wa
ushirikiano unaohusisha mwanafunzi, mwalimu pamoja na wazazi hao katika
kuendeleza mbele elimu.
‘’Wazazi
msiwaachie waalimu peke yao , na nyinyi mnapoitwa mje skuli kwani
kumtengeneza mwanafunzi, kunahitajika nguvu za pamoja na sio waalimu
peke yake’’,alifafanua Makamu huyo wa Kwanza wa rais Zanzibar .
Kuhusu
Dkahalia, alisema hata Serikali haijaridhika kwa skuli hiyo na nyengine
kukosekana kwakwe, na bado inaendelea kutafuta wafadhili, ili kuondoa
kero hiyo iliopo kwa muda mrefu.
Hata
hivyo amewataka wananchi kuelewa dhana ya elimu bure, ambayo iliasisiwa
na mwasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964, Amani Abeid Karume
na kuona umuhimu wake na wasisite kuchangia pale panaopohitajika.
Kwa
upande wake Naibu Ktaibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mfunzo ya Amali,
Abdalla Mzee, alisema skuli hiyo pekee, imegharimu jumla ya shilingi
Bilion moja, ikiwa ni fedha za mkopo kutoka benki ya dunia (WB).
Alisema
benki hiyo, ilikubali kuikopesha Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ,
jumla ya dola za Marekani 42 milion, sawa na shilingi 55 bilion, kwa
ajili ya ujenzi wa skuli 25 za Unguja na Pemba na chuo kimoja cha ualimu
Mzee
alifafanua kuwa kati ya dola hizo 42 milion, baada ya kutumia dola 32.9
bakaa ambayo inaendelea kutumiwa ni dola milion 9. 4, huku mazungumzo
ya awali yakiwa yameshafanyika bina ya benki ya dunia na Serikali juu
kupatiwa mradi mwengine utakaohusisha ujenzi wa dakhalia
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Juma Kassim Tindwa, alielezea
wasiwasi wake juu ya utunzaji wa majengo hayo, ambayo mara baada ya
wafadhili kuondoka huanza kupoteza hadhi yake.
Akisoma
risala katika hafka hiyo, Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Wawi Said Mohamed
ameiomba Serikali kuangalia uwezekano wa kuwapatia gari skulini hapo,
hasa kutokana na kuwa mbali na barabara kuu.
Jumla
ya wanafunzi 480 watafaidika ndani ya madarasa hayo 12 kwa wakati mmoja
katika skuli hiyo mpya ya sekondari ya Dk. Omar Ali Juma, ambayo pia
ina vyumba vitatu vya maabara, chumba kimoja cha kompyuta, ukumbi wa
mkutano, afisi za mwalimu mkuu na msaidizi wake.Na Haji Nassor, Pemba
No comments:
Post a Comment