Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr Shein akizindua rasmi Barabara ya Bumbwini-Mfenesini.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein
ameuagiza uongozi wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano kuziwekea
Mipaka maalum barabara zinazojengwa Zanzibar ili Wananchi waepuke
kujenga pembezoni mwa barabara hizo.
Hayo
ameyasema jana huko Bumbwini-Mfenisini wakati wa ufunguzi wa barabara
hiyo ikiwani ni mwendelezo wa shamra shamra za kutimiza miaka 49 ya
Mapinduzi ya Zanzibar.
Dkt.
Shein amesema kwa kufanya hivyo kutaisaidia Serikali kuepukana kuwalipa
fidia Wananchi ambao wanatabia za kujenga katika maeneo ya barabara kwa
kutarajia malipo pale nyumba zao zitakapobomolewa kufanya utanuzi wa
barabara hizo.
“Mnawachia watu wanajenga pembezoni mwa bara bara wakati mnawaona, mtu anaaza msingi, anainua tofali, anaezeka ,na anapiga palasta na nyinyi mnashuhudia,lazima iwekwe mipaka ya kuonesha eneo hili halipaswi kujengwa na atakae jenga avunjiwe .”alifahamisha Dkt.Sheini.
Wananchi mbali mbali waliofika kwa ajili ya kushuhudia sherehe hizo za uzinduzi wa Barabara
Dkt.
Shein alitoa mfano wa barabara zilizojengwa nyumba pembezoni ambazo
zinatarajiwa kutanuliwa siku za karibuni kuwa ni bara bara ya
Magomeni-Kwerekwe na barabara ya Bububu kuelekea Mkoa wa Kaskazini
Unguja.
Alisema
bara bara hizo ziliwekewa maeneo yake kwa ajili ya utanuzi siku za
usoni lakini hakukuwa na mkakati wowote wa kulinda mipaka ya barabara
hizo jambo ambalo liliwapelekea wananchi kupuuza sheria kwa kujenga
nyumba.
Aidha
Dkt. Shein aliwataka watendaji wa Wizara hiyo kuzitunza vyema Bara bara
hizo alizozizindua pamoja na Madaraja manne ikiwa ni pamoja na kupanda
miti pembezoni na kuepusha kuchomwa moto kwa kutumia matairi ili
zisipoteze kiwango chake.
Nae Mwakilishi mkazi kutoka AFDB Bank Bi Toniya Kandiyero alisema kuwa Bank yao ipo mstari wa mbele kusaidia maendeleo ya Zanzibar katika miradi mbalimbali ambapo kwa upande wa Barabara imesaidia takribani Kilomita 83 katika maeneo ya Unguja na Pemba.
Bi
Toniya alisema kwa sasa benki yake imejipanga kusaidia maeneo mengine
mapya kama vile mazingira ya bahari na raslimali zake pamoja na shughuli
zinazo fanywa baharini.
Baadhi ya viongozi mbali mbali wa Serikali wakiwa kwenye picha ya pamoja kuadhimisha shughuli nzima ya uzinduzi wa Barabara
No comments:
Post a Comment