
Jan
9
2013
MWANDISHI wa Habari wa Kituo cha Redio Kwizera wilayani Kakonko, Mkoa
wa Kigoma, Issa Ngumba (45), ameuawa kwa kupigwa risasi na kunyongwa na
watu wasiofahamika.
Habari zilizopatikana jana zimeeleza kuwa mwili wa mwandishi huyo
ulikutwa porini, siku tatu tangu alipotoweka nyumbani kwake katika
mazingira ya kutatanisha.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Frasser Kashai alithibitisha tukio
hilo, lakini akasema asingeweza kulizungumzia kwa undani kwa kuwa polisi
walikuwa bado eneo la tukio.
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wamesema mwandishi huyo alikutwa
jana akiwa amekufa, huku mwili wake ukiwa na majeraha ya risasi na ukiwa
umenyongwa na pembeni yake kulikuwa bastola iliyokuwa imetelekezwa
pamoja na simu zake mbili za mkononi.
“Mwili wake ulipatikana jana katika Pori la Mlima Kajuluheta ulioko
katika Kijiji cha Muhange, Kakonko asubuhi baada ya wananchi kufanya
msako wa siku tatu tangu Jumapili iliyopita ikiwa ni siku moja baada ya
kupotea katika mazingira ya kutatanisha,” alisema mmoja wa mashuhuda
hao.
Imeelezwa kuwa pamoja na vifaa hivyo, pia katika eneo hilo la tukio
kulikutwa risasi tano na katika mfuko mmoja wa suruali ya marehemu,
kulikuwa na noti moja ya Sh10,000.
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Kigoma (KPC) Deogratius
Nsokolo alisema: “Sisi ndiyo kwanza tunaelekea eneo la tukio, lakini
waandishi wa Wilaya ya Kibondo ambao waliwahi kufika eneo la tukio na
kushuhudia uchunguzi wa daktari, wameeleza kuwa marehemu amekufa kwa
kunyongwa na kupigwa risasi mkono wa kushoto.”
“Tunaelekea Wilaya ya Kakonko kutoka Kigoma Mjini, lakini daktari
amesema maiti inaonekana kunyongwa shingo na kupigwa risasi mkononi.”
Alisema mwili huo ulifanyiwa uchunguzi na daktari Primus Ijumaa wa Hospitali ya Wilaya ya Kibondo.
Kamanda Kashai alisema jeshi lake linasubiri taarifa ya daktari
aliyefanya uchunguzi wa mwili wa marehemu pamoja na taarifa za awali za
uchunguzi kabla ya kutoa taarifa kamili kwa waandishi wa habari.
Naibu Mhariri wa Kituo cha Redio Kwizera kinachorusha matangazo yake
kutoka wilayani Ngara mkoani Kagera, Seifu Upupu alisema mwandishi huyo
alipotea tangu Januari 5, mwaka huu saa kumi na moja jioni.
“Simu zake zilikuwa zikiita bila kupokewa kwa muda wote na hadi jana
(juzi) zikawa hazipatikani kabisa,’ alisema Upupu na kuongeza:
CHANZO MWANANCHI
CHANZO MWANANCHI
No comments:
Post a Comment