Saturday, January 26, 2013

Huduma ya wanyamapori nchini Kenya imeweka mifumo ya kamsa kuzunguka hifadhi ya wanyama pori ili kuzuia ujangili

Shirika la Wanyamapori nchini Kenya (KWS) linafunga mfumo wa kamsa kuzunguka hifadhi ya wanyama pori na mbuga ili kuzuia kuongezeka kwa ujangili unaoenea katika nchi.
  • Waajiriwa wa Mamlaka ya Bandari ya Kenya wakipima pembe za ndovu tarehe 21 Januari katika bandari ya Mombasa. Mamlaka ya Mapato ya Kenya ilikamata kontena hapo tarehe 15 Januari ambalo lilikuwa na pembe za ndovu 638, usafirishaji wa mzigo ulio mkubwa kabisa katika nchi kwenye kumbukumbu. [Ivan Lieman/AFP] Waajiriwa wa Mamlaka ya Bandari ya Kenya wakipima pembe za ndovu tarehe 21 Januari katika bandari ya Mombasa. Mamlaka ya Mapato ya Kenya ilikamata kontena hapo tarehe 15 Januari ambalo lilikuwa na pembe za ndovu 638, usafirishaji wa mzigo ulio mkubwa kabisa katika nchi kwenye kumbukumbu. [Ivan Lieman/AFP]
  • Wahamasishaji wakishiriki katika maandamano hapo tarehe 22 Januari jijini Nairobi kuweka msukumo kwa serikali kutamka wazi ujangili unaoendelea wa vifaru na tembo kama janga la kitaifa. Mkurugenzi wa Huduma ya Wanyamapori ya Kenya William Kibet Kiprono anakadiria kuwa ujangili umeongezeka kwa asilimia 33 kutoka mwaka 2011 hadi 2012. [Tony Karumba/AFP] Wahamasishaji wakishiriki katika maandamano hapo tarehe 22 Januari jijini Nairobi kuweka msukumo kwa serikali kutamka wazi ujangili unaoendelea wa vifaru na tembo kama janga la kitaifa. Mkurugenzi wa Huduma ya Wanyamapori ya Kenya William Kibet Kiprono anakadiria kuwa ujangili umeongezeka kwa asilimia 33 kutoka mwaka 2011 hadi 2012. [Tony Karumba/AFP]
Mkurugenzi wa KWS William Kibet Kiprono alisema mifumo ya kamsa itawatahadharisha wasimamizi wa hifadhi za wanyamapori kuhusu uingiaji katika mbuga za wanyama.
"Mfumo huu utaweza kuzuia ujangili kwa angalau asilimia 90," aliiambia Sabahi. "Tunahisi kwamba hili ni suluhisho la muda mrefu kuokoa wanyama wetu ambao wanatoweshwa na majangili."
Katika matukio ya hivi karibuni ya ujangili, tarehe 5 Januari, majangili yaliua familia ya tembo 11 na kuondoa pembe zake katika mbuga ya wanyama ya Taifa mashariki mwa Tsavo katika jambo ambalo maofisa walisema lilikuwa tukio baya sana kwa nchi katika miongo mitatu. Siku kumi baadaye, maofisa jijini Mombasa walikamata tani mbili za pembe za ndovu usafirishaji ulio mkubwa kabisa nchini Kenya katika kumbukumbu.
Kuongezeka katika idadi ya matukio ya ujangili katika kanda kutokana na uhitaji kunatokana na kustawi kwa soko haramu la pembe za ndovu barani Asia.
Biashara ya kimataifa ya pembe za ndovu, kukiwa na tofauti kidogo, ilipigwa marufuku mwaka 1989 baada ya idadi ya tembo katika Afrika kupungua kutoka mamilioni katikati ya karne ya 20 hadi 600,000 mwishoni mwa miaka ya 1980.
"Wanyama hawa wanaelekea katika kundi la jamii ya wanyama walio katika hatari -- mwelekeo huu haukubaliki na hauwezi kuvumiliwa zaidi" Kiprono alisema. "Hiyo ndiyo sababu tumekuja na mbinu nyingine zaidi kushughulikia hali hii inayotishia. Mwaka uliopita, tulipoteza zaidi ya tembo 384 na vifaru 19; mwaka 2011 tulipoteza tembo 289 na vifaru 29. Mwezi huu pekee, tuna tembo zaidi ya 15 na vifaru saba waliouawa.

KWS kuajiri wasimamizi zaidi wa hifadhi za wanyama

Kamsa zinazofungwa katika uzio wa mbuga za wanyama zitatoza sauti pale zitakapochezewa, pamoja na kutuma ujumbe wa maandishi kwenye swichibodi.
"Kuchezea uzio kutajumuisha kuingiliana na wanyama na majaribio ya majangili kuvamia uzio," alisema. "Ishara hiyo itaonyesha eneo hasa kwa hiyo msimamizi wa mbuga atalifanyia kazi kwa wakati".
Kiprono alisema KWS inatafuta kuboresha uwezo wake kwa kuajiri wasimamizi wa hifadhi za wanyama pori zaidi ya wasimamizi 800 na kufunza jamii zinazoishi maeneo ya karibu na mbuga za wanyama namna ya kuhusishwa katika vita dhidi ya ujangili.
"Pia tutanunua ndege, bunduki na magari kuwezesha na kurahisisha harakati za maofisa wetu," alisema, kukataa madai kwamba kuna utaratibu unaokwenda polepole miongoni mwa wasimamizi wa hifadhi za wanyama pori wa KWS ambao unaweza kuzidisha tatizo la ujangili.
Alisema kama sehemu ya mipango yake ya kina, shirika limetoa kazi mwezi Agosti ya ujenzi wa maabara za kuchunguza vitu vya kupelekwa mahakamani na vya kijenetiki vya wanyama pori iliyo ya kwanza katika kanda makao makuu jijini Nairobi. Wakati itakapomalizika, maabara hiyo itasaidia uchunguzi kuendesha kesi za uhalifu unaohusishwa na wanyamapori, kutafuta hali ya kijenetiki ya wanyamapori waliyotoweka, na kuamua aina ya jene ambayo inahitaji mashtaka maalumu.
Tarehe 20 Januari, Mkuu wa Huduma za Umma wa Kenya Francis Kimemia alisema alielekeza KWS kuchunguza tuhuma kwamba waangalizi wa awali walijiunga na magenge ya uhalifu kutoka Somalia na walihusika katika ujangili.
"Wanapaswa kumpa rais ripoti ya jinsi tunavyoendelea kupoteza idadi kubwa ya wanyama pori -- urithi wetu -- na kwa nini imeenea ndani ya hifadhi binafsi, nani anayehusika, na kwa nini wameshindwa kuzuia na kutunza hifadhi zetu," alisema katika taarifa.
Kiprono aliiambia Sabahi kwamba uchunguzi umefikia katika hatua ya juu lakini alikataa kueleza kwa undani.

Ujangili unatishia utalii

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Utalii Kenya Agatha Juma alisema shirika lilipatwa na wasiwasi kutokana na ongezeko la matukio ya ujangili, ambayo alisema yanaweza kuua utalii.
"Uti wa mgongo wa sekta ya utalii ya Kenya unaegemea katika safari za kuona wanyama pori, na kama tutaruhusu tembo na vifaru wetu kuuawa, hatimaye tujue kwa hakika kwamba hakuna mtaalii atakayetembelea Kenya,” alisema.
Huku akiunga mkono mpango mpya wa uchunguzi utakaofanywa na KWS, pia aliliomba shirika kuwawezesha waangalizi wa wanyama pori kwa kuwapa silaha ili kukabiliana na majangili ambao wanatumia bunduki za kisasa.
Michael Mutua, mwendeshaji wa watalii katika Wildlife Sun Safaris, alisema kupungua kwa idadi ya tembo na vifaru katika mbuga tayari kunapunguza mvuto wa kuenda kwenye hifadhi ya wanyama.
Mwezi Disemba, niliwachukua baadhi ya watalii kutoka Italia hadi Amboseli kuona wanyama wakubwa watano -- simba, chui, tembo, nyati na vifaru. Tulitumia siku nzima kuwatafuta wanyama hao bila mafanikio, hivyo, walikasirishwa na kuamua kuondoka," aliiambia Sabahi. "Walikata tiketi ya ndege iliyokuwa ikitoka siku hiyo ili kumalizia utalii wao huko Afrika Kusini."
Alitoa wito kwa serikali kuwekeza katika teknolojia nyingine kama vile droni ambayo inaweza kumfuatilia mtu na kuwazuia majangili.
Awali, watembeza watalii walihitaji chini ya dakika 30 kuwatafuta wanyama, lakini kwa sababu ya kuenea kwa uuaji wa tembo na vifaru, wanyama wanajificha mbali na njia za magari, alisema Mutua.

No comments:

Post a Comment