Wednesday, January 30, 2013

JUSSA AMSHAURI DR:SHEIN KUBADILISHA BARAZA LA MAWAZIRI


 
 
 
 
 
 
Rate This

Imewekwa na Hamed Mazrouy
Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe Ismail Jussa akiwa ndani ya Baraza la Wawakilishi
Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe Ismail Jussa akiwa ndani ya Baraza la Wawakilishi
Mwakilishi wa jimbo la Mji Mkongwe Mh: Ismail Jussa amemshauri Rais wa Zanzibar Dr, Ali Mohamed Shein  kuvunja Baraza zima la Mawaziri wake waliomo ndani ya Serikali hii ya Zanzibar kwani  wamekuwa wakishindwa katika suala zima la utekelezaji wa majukumu yao ya kazi kama wahusika wakuu wa Wizara zao.

Hayo yamekuja kufuatia Mwakilishi huyo alipopata nafasi ya kuchangia moja miongoni mwa hoja zilizo wasilishwa  huko ndani ya Baraza la wawakilishi lililopo Chukwani nje kidogo ya mji wa Zanzibar, iliyokuwa inahusiana na  na kamati kadhaa zilizowahi kuundwa ndania ya Baraza hilo kwa ajili ya uchunguzi  wa mambo mbali mbali hapa Nchini.


Jussa amesema kuwa anashangazwa kuona ndani ya Serikali hii  Mawaziri waliochaguliwa na kuaminiwa kushindwa hata kuandika Ripoti ya utekelezaji wa maepndekezo ya kamati za Baraza la Wawakilishi zilizoundwa kwa ajili ya kuchunguza.

Sambamba na hayo Mh:Jussa ametolea mfano kuwa Mawaziri hao  wameshindwa hata kuandika ripoti ya utekelezaji wa mapendekezo ya kamati za baraza zilizoundwa,akitolea mfano amesema kuwa hadi leo hii ambapo takribani ni ripoti ya tatu inawasilishwa lakini bado utekezaji wake haujaonekana mpaka sasa.

Aidha amefahamisha kuwa kuhusu suala la ripoti ya pili ambayo utekelezaji wake ni wa kusuasua haikuonyesha kama mawaziri wa Serikali hii wapo  seriou katika kazi zao hivo basi kitendo cha Mawaziri hao kuwasilisha vikaratasi   viwili vitatu haioneshi kuwa ndio utekelezaji wao hivo basi kutokana na hatuwa hio hakuoneshi wala kutia sura nzuri na kufanya maswali yazidi kuwa mengi kwao kuliko majibu ya uwezo wao.

No comments:

Post a Comment