Wednesday, January 30, 2013

Mzozo Syria wafikia kiwango cha kutisha

 30 Januari, 2013 - Saa 07:46 GMT

Mjumbe maalum wa Umoja wa mataifa nchini Syria , Lakhdar Brahimi, ameliambia baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuwa mzozo nchini Syria umefikia kiwango cha kutisha ambacho hakijawahi kushuhudiwa.
Bwana Ibrahim amesema kuwa Syria inaangamizwa siku hadi siku kuhu athari kubwa zikiwa ni kwa kanda nzima , na kwamba baraza la usalama lenye mgawanyiko linapaswa kuchukua hatua .
Alikuwa akitoa mfano juu ya kushindwa kwa baraza hilo kuafikiana ikiwa rais Assad anapaswa kushirikishwa katika kipindi cha mpito cha kisiasa au la.
Kauli ya Mjumbe huyo wa Umoja wa mataifa imetolewa saa kadhaa baada ya watu kadhaa kukutwa wameuawa katika mji wa Aleppo.
Imebaini ka kuwa waliuawa wakati mmoja. Serikali na Upinzani kila upande umekuwa ukimlaumu mwenzake kwa mauaji hayo. Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa zaidi ya watu elfu 60,000 wamekwishauawa nchini Syria tangu mzozo ulipoanza mwezi March 2011

No comments:

Post a Comment