Wednesday, January 30, 2013

Kesi kuhusu Shell Nigeria kuamuliwa leo

 30 Januari, 2013 - Saa 08:15 GMT
Wakulima walioshtaki kampuni ya Shell

Mahakama ya viwanda nchini Hague hii leo inatarajiwa kutoa uamuzi juu ya kesi iliyowasilishwa na wakulima kutoka Nigeria dhidi ya kampuni ya mafuta ya Shell.
Hatma ya kesi hiyo inatazamiwa kutoa mwelekeo katika kesi zingine nyingi kama hiyo. Hii ni mara ya kwanza kwa kampuni kubwa ya kimataifa ya mafuta kushitakiwa kwa uharibifu wa mazingira hasa katika nchi za nje ya Uholanzi.
Kesi hiyo iliwasilishwa mahakamani na wanaharakati wa kutetea mazingira (Friends of the Earth,) pamoja na raia wanne wa Nigeria waliotaka kulipwa fidia kwa hasara waliyopata.
Wanne hao ambao ni mkulima na mvuvi, wanasema kuwa mafuta yalivyovuja kutoka kwa mabomba ya mafuta ya kampuni ya Shell, yaliharibu ardhi na vyanzo vya maji, katika eneo la Niger Delta, na kuwazuia kulisha familia zao kutokana na athari zake.
Kampuni ya Shell inasema kuwa kuvuja kwa mafuta kulisababishwa na vitendo vya wizi na hujuma na kwamba wamejaribu kusafisha mazingira.
Uamuzi wa mahakama hii leo, huenda ukawa tahadhari kwa makampuni ya kigeni kuwajibikia vitendo vyao katika nchio za kigeni hasa barani Afrika.
Mawakili wanne wa Nigeria, kutoka eneo lenye utajiri mkubwa wa mafuta la Niger Delta wanasema kuwa kampuni ya Shell hubuni sera zake kuu katika makao yake makuu mjini Hague na hivyo ni sawa kwa mahakama ya Uhalonzi kusikiliza kesi hiyo.
Ingawa Shell ilikuwa imesisitiza kuwa kesi hiyo iliyowasilishwa mahakamani mwaka 2008,ingepaswa kusikilizwa nchini Nigeria.
Hii bila shaka ni kesi ya kwanza kuhusisha kampuni ya mafuta ya Shell kushtakiwa juu ya madai ya uharibifu wa mazingir

No comments:

Post a Comment