Friday, January 4, 2013

Kuongezeka kwa uingiaji kwenye intaneti nchini Kenya kunatoa kazi, kuimarisha elimu

Unganishwaji wa intaneti ulioboreshwa nchini Kenya unaongeza ukuaji wa uchumi, kupatikana kwa kazi na kuongeza upataji wa elimu, maofisa wahusika wa tasnia hiyo wamesema.
  • Mem Maina akionyesha matumizi ya simu mpya wakati wa maonyesho ya teknolojia ya Afrika ya DEMO kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Kenyatta jijini Nairobi tarehe 25 Oktoba. Utafiti wa hivi karibuni ulionyesha kwamba simu za mkononi zinaweza kusaidia kuondoa pengo linalotenganisha la dijitali na kutoa ufikivu wa intaneti kwa Wakenya wengi zaidi. [Simon Maina/AFP] Mem Maina akionyesha matumizi ya simu mpya wakati wa maonyesho ya teknolojia ya Afrika ya DEMO kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Kenyatta jijini Nairobi tarehe 25 Oktoba. Utafiti wa hivi karibuni ulionyesha kwamba simu za mkononi zinaweza kusaidia kuondoa pengo linalotenganisha la dijitali na kutoa ufikivu wa intaneti kwa Wakenya wengi zaidi. [Simon Maina/AFP]
Huduma za mtandao zinazopatikana kwenye kompyuta na simu za mkononi zimepunguza gharama za muamala katika sekta mbalimbali na kusaidia kufanya maisha ya raia kuwa rahisi, kwa mujibu wa mwenyekiti wa Chama cha Walaji cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) Alex Gakuru.
"Wananchi wanaweza kupakua na kujaza nyaraka muhimu kama vile ripoti ya polisi kwa kubofya kipanya," aliiambia Sabahi. "Wanaweza kulipa bili kwa kutumia simu zao za mkononi na wanaweza kuomba kazi kupitia mtandao. Hii inamaanisha kwamba inapunguza kusafiri na matumizi."
Kwa mujibu wa ripoti ya Tume ya Mawasiliano ya Kenya ya 2011-2012 iliyotolewa Oktoba, matumizi ya intaneti kupitia kompyuta za kawaida yamekua kwa watumiaji milioni kwa silimia 19.2 hadi 7.7, wakati matumizi ya inteneti kwa njia ya simu za mkononi yamekua kwa watumiaji milioni kwa asilimia 1.7 hadi 29.7.
Ingawaje gharama kubwa za ufikiaji zimeendelea kuwepo, Gakuru alisema, kuogezeka kwa uingiaji kwenye intaneti umeboresha biashara, mawasiliano na mandhari ya elimu nchini Kenya.
Uunganishwaji mzuri umetafsiriwa kwenye gharama ndogo za matangazo kwa ajili ya biashara, kwani sasa wanaweza kufikia watu wengi kupitia mtandao. Kuwasiliana na wateja kupitia mtandao, ambao wanatoa mwitikio kwa wamiliki wa biashara, husaidia malengo ya kampuni na kukidhi vizuri matakwa ya wateja, Gakuru alisema.

Upatikanaji wa intaneti unaimarisha kujifunza, kuleta ajira

James Ratemo, mhariri wa mtandao na vyombo mbalimbali vya habari anayefanyia kazi gazeti la Daily Nation huko Nairobi, alisema teknolojia inayozingatia intaneti inafanya kujifunza kuwe kwa mwingiliano zaidi na kuvutia, ambako kunawasaidia wanafunzi kupata maarifa kwa urahisi zaidi.
Serikali imeendeleza mtindo huu unaoibuka kwa kuanzisha programu za kujifunza kupitia elektroni katika shule ambako kunasaidia kusimamia vizuri na kuyafanya madarasa ya Kenya kuwa ya kisasa na kuwafundisha wanafunzi teknolojia mpya, alisema.
Peter Agira, mwalimu wa hisabati katika Shule ya Msingi ya Rudolf Steiner, Nairobi, alisema kujumuisha teknolojia mpya darasani kumewasaidia walimu katika shule yake kusimamia vizuri kazi maalumu kwa wanafunzi wao na kufuatilia maendeleo yao.
"Matumizi ya kompyuta na tablets yamechochea kupenda kujifunza," alisema. "Matumizi ya vyombo vya dijitali badala ya mbao za kutumia chaki na madaftari kumefanya kujifunza kwa wanafunzi wetu kuwe kwa kuvutia, ambako kumekuwa msaada katika kufundisha hesabu ngumu."
Mtendaji mkuu wa Bodi ya TEHAMA ya Kenya Paul Kukubo alisema kuboreka kwa upatikanaji wa intaneti kumesaidia kupatikana kwa kiasi cha ajira 1,000 kila mwezi katika mchakato wa biashara wa sekta kutoka nje.
Alisema Bodi ya TEHAMA ilizindua programu ya kompyuta ya mtihani kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Carnegie Mellon huko Marekani ambayo ililenga kuthibitisha waandaaji 500 wa programu za kompyuta Kenya kila mwaka. Programu unalenga kuwasaidia wataalamu kupata vyeti vinavyotambulika kimataifa vinavyotakiwa katika kuendeleza matumizi ya programu za kompyuta Kenya na kuleta ajira.
"Kenya inaendelea kwa haraka kama kituo cha kuandaa programu za kompyuta, hasa wakati linapokuja suala la matumizi ya simu za mkononi," Kukubo alisema. "Serikali inaimarisha hilo kwa msaada wa kuwe vituo vya kipindi cha ukuzaji ambapo vyanzo muhimu vinaweza kusaidiwa."

Kuunganisha mgawanyo wa intaneti

Pamoja na matokeo chanya ambayo yameleta kasi kubwa ya intaneti katika uchumi wa Kenya, tofauti katika upatikanaji inabaki kuwa kikwazo kikubwa, kwani watumiaji wengi wa intaneti wapo jijini Nairobi.
"Kushughulikia masuala ya dijitali kutasaidia watu wa vijijini kuunganishwa," alisema Gakuru wa Chama cha Watumiaji wa TEHAMA. "Hili litawasaidia kushiriki katika shughuli za kiuchumi kama vile kutafuta masoko kwa ajili ya bidhaa zao za kilimo kwa urahisi zaidi na kwa gharama ndogo."
Simu za mkononi zitasaidia kuunganisha dijitali na kutoa upatikanaji wa intaneti kwa Wakenya wengi, kwa mujibu wa Utafiti wa Watumiaji wa Simu za Mkononi, uliofanyika mwezi Novemba na iHub, kituo cha ugunduzi wa teknolojia kilichopo Nairobi.
Hata hivyo, uwezekano huu ulizuiliwa na gharama kubwa ya data zinazowezesha bei za simu za mkononi na gharama za mpango wa data ambazo zinatozwa kwa Wakenya wengi.
Gakuru anasema njia pekee ya kushughulikia mgawanyiko wa dijitali ni kupitia jitihada endelevu, kama vile kwa kuongeza kodi kwa makampuni ya mawasiliano ya simu ambayo yanatoa huduma katika majiji na kupunguza kozi kwa waendeshaji wanaounganisha maeneo ya vijijini katika intaneti.
Mwandishi wa habari Ratemo alisema serikali inapaswa kusimamisha kodi katika simu ili kuzifanya kuwa za bei nafuu ili wananchi katika maeneo ambayo uunganishaji kwa njia ya kebo haupo waweze kuunganishwa kwa kupitia simu.
"Kama bei za simu zitapunguzwa kwa kiasi kikubwa, itamaanisha kwamba wakulima wote wa Kenya, au hata washona viatu, watakuwa na uwezo wa kumiliki simu zenye uwezo wa kupata intaneti, na kwa hiyo watakuwa na uwezo wa [kutafuta] masoko ya bidhaa zao kwa kutumia simu zao za mkononi," alisema, akiongeza kwamba serikali na watoa huduma ya simu za mkononi wanapaswa kushirikiana kushusha gharama za data.
Kukubo alisema serikali inakamilisha jitihada za uunganishaji wa nchi kuhakikisha kila eneo kati ya mikoa 47 ya Kenya limeunganishwa kikamilifu katika kebo ya mtandao wa taifa. Kukamilisha kazi ya awali ya miundombinu hiyo kutasaidia kuongeza uunganishwaji katika nchi nzima na kuunganisha mgawanyo huo, alisema.

No comments:

Post a Comment