Wizara ya Habari na Mawasiliano ya Kenya imewapa raia hadi Ijumaa
(tarehe 4 Januari) kusajili laini zao za simu za mkononi, liliripoti
gazeti la The Standard la Kenya.
“Tunao hadi hapo Ijumaa na kila mtu afahamu kwamba madhara ya
kutosajili utakuja kuwagharimu shilingi 300,000 (dola 3,500) au miaka
mitatu jela,” alisema Katibu Mkuu Bitange Ndemo. “Kanuni tayari zipo
kwenye ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali na notisi ya kisheria
itatangazwa kwenye gazeti Ijumaa.”
Muda wa mwisho wa kusajili ulikuwa ni Jumatatu, huku serikali
ikitishia kuzifungia nambari zote zisizosajiliwa, lakini hakuna
iliyozimwa hadi sasa.
Ndemo alisema hatua hiyo ya kuzichukulia hatua namba zisizosajiliwa
ni muhimu kwa kuhakikisha msimu salama wa uchaguzi, ukiwawezesha polisi
kufuatilia ujumbe unaochochea ghasia na kuwakamata wahusika, kiliripoti
kituo cha Capital FM cha Kenya.
Kuna laini za simu milioni 30.8 zinazofanya kazi nchini Kenya,
asilimia 80.4 zikiwa zimesajiliwa, kwa mujibu wa Kamisheni ya
Mawasiliano ya Kenya.
No comments:
Post a Comment